Sunday, January 12, 2014

MUNDE AWATAKA WANAWAKE KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI VYA UJASILIAMALI.

 

 

Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Tabora Bi.Munde Tambwe amewaasa wanawake mkoani humo kujiunga katika vikundi vya wajasiliamali ili waweze kukopesheka hatua ambayo itasaidia kumkomboa mwanamke kiuchumi,Mheshimiwa Munde Tambwe ambaye amekuwa na msimamo na malengo mahususi ya  kuwasaidia wanawake mkoani Tabora ameahidi kuendelea kufanya hivyo huku akisisitiza wanawake hao kumuunga mkono kwa kujiunga katika vikundi ambavyo wataanzisha shughuli mbalimbali za maendeleo yao.Pamoja na juhudi zinazooneshwa na mbunge huyo kama alivyoahidi wakati akiomba ridhaa ya kupata wadhifa alionao amesema tayari amekwisha saidia na kufadhili mafunzo kwa wajasiliamali wanawake yatakayosaidia kuondokana na umasikini wa kipato unaowakabili.  

No comments:

Post a Comment