Friday, January 31, 2014

"MWAKASAKA AMRITHI MWALIMU NYERERE"


Mjumbe wa halmashauri kuu na kamati kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Emmanuel Adamson Mwakasaka hivi karibuni alitawazwa kuwa Mlezi wa Jamii ya Waswezi mkoa wa Tabora ambapo ameshika wadhfa huo akiwa ni mtu wa pili baada ya Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye alitumikia nafasi hiyo enzi za uhai wake wakati wa harakati za kusaka uhuru wa Tanganyika hadi alipofariki dunia.Mwakasaka amepewa heshima ya kushika nafasi hiyo akiwa ni mtu wa pili  baada ya Mwalimu Nyerere.
Bw.Mwakasaka akikabidhiwa Usinga wa Kiswezi(kifaa cha matambiko)na mkuki ikiwa ni ishara ya kutawazwa kuwa kiongozi mlezi wa Waswezi Tabora.

No comments:

Post a Comment