Tuesday, August 20, 2013

MBOWE;KATIBA HAINA DINI,RANGI,KABILA




NA LUCAS RAPHAEL NZEGA 

MWENYEKITI wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa katiba haina dini,rangi wala ukabila kutokana na umuhimu wake kwa maisha ya wananchi ya kila siku.

Akiwahutubia wananchi wa Nzega mjini katika viwanja vya parking jana alisema kuwa wananchi wanapaswa kutoa maoni yao dhidi ya rasim ya katiba kabla ya Agust 30 mwaka huu.

Alisema chama hicho kinapiga kampeni ya kuhamasisha waTanzania kuangalia mambo ya msingi katika katiba hiyo ambayo yataleta tija kwa wananchi ilikatiba ijayo iwena masirahi kwa wananchi wote.

Alisema kuwa endapo wananchi wakipuuzia ushauri huo utawagharim kwa miaka kadhaa na kusababisha hali mbaya ya maisha dhidi ya katiba itakayo pita.

Alisema kuwa mchakato huo wa kukusanya maoni ya katiba hauna itikadi ya kisiasa,Dini,rangi wala kabila bali ni masirahi ya wananchi wote hapa nchini ambapo wanapaswa kutoa ushirikiano wa kutosha ilikuweza kupata katiba itakayo wasaidia katika maisha yao.

Alisema kuwa watanzania waliobahatika kutoa maoni ya katiba katika duru ya kwanza ni wachache kuliko idadi iliyopo na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa watoe maoni yao katika kupata katiba waitayo yenye masirahi ya msingi kwa kila mtanzaia.

Mwenyekiti huyo aliipongeza Tume ya mabadiliko ya katiba inayongozwa na mwenyekiti wake Jaji sinde warioba kuwa imetoa rasimu ya msingi yenye maoni ya watanzania na kuongeza kuwa baadhi ya vyama vya siasa vinafanya utaratibu wa kuipinga rasim hiyo baadhi ya vipengele.

Kwa upande wake mnadhimu wa kambi ya upinzani Tundu Lisu alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM kinampango wa kupinga baadhi ya vipengele ikiwepo na mfumo wa serikali tatu.

Alisema kuwa maoni ya wananchi yaheshimiwe kimsingi kutokana na rasimu hiyo ya katiba hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kutoa maoni yao dhidi ya rasimu hiyo ya katiba.

Lisu alisema kuwa katika Bunge la katiba lijalilo litakuwa halitoshi kutokana na kuhakikisha haki za wananchi zinapatiwa ufumbuzi wa kutosha ili kila maoni ya msingi yawqeze kupita.

Alisema kuwa watahakikisha vipengele vyote vinasimamiwa kikamilifu kwa kuzingatia sheria na utaratibu na kuongeza kuwa wananchi wazingatie mambo yao ya msingi waliyoyataka katika maoni.

Shuguli za uzalishaji mali nzega mjini ikiwepo kufungwa kwa maduka,soko zilisimama zaidi ya masaa sita kutokana na wananchi kukusanyika kwa wingi kusubili msafara huo wa mwenyekiti wa chama hicho pamoja na mnazimu wa kambi ya upinzani Tundu Lisu.

Mwisho.


No comments:

Post a Comment