Saturday, August 10, 2013

MWAKASAKA ATOA MSAADA WA VITU VYA ZAIDI YA SHILINGI MIL.NANE TABORA GIRLS


 

Mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm wilaya ya Tabora mjini Bw.Emmanuel Mwakasaka  akikabidhi  moja ya seti tatu za kompyuta alizotoa msaada kwa Shule ya Sekondari ya Tabora Wasichana,msaada huo ni pamoja na Jenereta na Projector wenye thamani ya zaidi ya shilingi mil.nane na nusu.
Jenereta iliyotolewa msaada  kwa Shule hiyo.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Tabora mjini  Mwalimu  Lucas Masanja akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo.




  
 NA LUCAS RAPHAEL TABORA

WANAFUZI wa shule  ya sekondari ya wasichana, (Tabora Girls), wameiomba Serikali ijenge uzio katika shule hiyo ili kukomesha  matukio ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kila mara shuleni hapo.


Kilio hicho walikitoa jana muda mfupi baada ya kupokea msaada wa vifaa vya masomo, vilivyotolewa na mdau wa elimu Emmanuel Mwakasaka, katika hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Tabora.

Vifaa hivyo ni kompyuta tatu, Projekta moja na Jenereta moja, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 8.4.

Katika Risara yao iliyosomwa na Edina Marisa, wanafunzi hao walisema kuwa wanaiomba serikali na wadau hao wa elimu wenye mapenzi mema kwa shule hiyo kujiokeza kutoa michango ya fedha ili ziweze kutumika kujenga uzio huo kwa ajili ya usalama wa wananfunzi pamoja na mali za shule.

“Ndugu mgeni Rasmi shule yetu inakabiliwa na tatizo la kutokuwa na uzio kwa muda mrefu sasa, hivyo tunakuomba wewe pamoja na wenzako mtusaidie kujenga uzio, maana hapa tumekuwa tukivamiwa kila mara na wezi” ilisema sehemu ya risara hiyo.

Wameeleza kwamba kutokana na kutokuwepo kwa uzio huo, imekuwa ni rahisi kwa wezi na vibaka kuingia katika eneo la shule kufanya uhalifu na hivyo kupelekea wanafuzi kuishi kwa hofu kubwa ya kuvamiwa na vibaka hao ambao wamekuwa wakivamia shuleni hapo kila mara na kuwapora vitu kadhaa na kuwafanyia vitendo vya udharirishaji wa kijinsia.

Mbali na hayo pia wamesema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa mabweni ya kulala, ukosefu wa vifaa vya kujifunzia, uchakavu wa madarasa na kuwepo mazingira hatarishi.

Kwa upende wake Mwalasaka ambaye pia mjumbe Halamshauri kuu ya CCM mkoani tabora,  alisema kuwa ameamua kutoa msaada huo baada ya kuguswa na hali haluisi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo yenye historia kubwa hapa nchini pamoja na wanafuzi wake.

“Kutoa nimoyo siyo utajili mimi nimeamua kusaidia hivi vitu kwa mapenzi yangu mwenyewe, sikuombwa na mtu wala kushawishiwa” alisema Mwakasaka.

Mwakasaka ametoa wito kwa wadau wengine wa elimu kujitokeza kutoa misaada mbalimbali kwenye shule hiyo, huku Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini Moshi Nkonkota akiwataka viongozi waliosoma katika shule hiyo nao wachangie fedha ili ziweze kutatua changamoto hizo.

Aliwataka mawaziri, mabalozi, makatibu wakuu wa wizara, na wabunge waliosoma shuleni hapo kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa shule inatatua matatizo yake.


Nkonkota alisema kuwa niabu kubwa kuona shule hiyo yenye historia ya kusoma viongozi wa serikali nchini, kukosa uzio wakati wao wangari wapo na wanauwezo mkubwa wa kunya hivyo.

Shule ya maalum ya sekondari ya wasichana Tabora (Tabora Girls) ilianzishwa mnamo mwaka 1928.

Mwisho   



No comments:

Post a Comment