Sunday, August 11, 2013

“NITAKUWA NAIBU MEYA WA WANANCHI NA SIO MPIMA VIWANJA NA KUSABABISHA MIGOGORO YA ARDHI”


Bw.Salumu  Msamazi diwani wa Kata ya  Ikomwa Manispaa ya Tabora.



Nashukuru  madiwani wenzangu pamoja na  viongozi wa CCM kwa  nafasi  zao,wameweza kunipigania hata kufikia  hatua  ya  kushinda  katika  uchaguzi  huu  wa  kumpata  mgombea  mmoja  kutoka  ndani  ya  chama chetu  atakaye  wania  nafasi  hii  adhimu  ya  Unaibu  Meya  wa  halmashauri  ya  manispaa  ya  Tabora.

Licha ya kuwa kulikuwa na makambi ambayo yalitupeleka kubaya lakini wadau  wangu  walikuwa  imara  kuhakikisha  hawawezi  kubadili  msimamo  wao  juu  yangu  na  kuhakikisha  wananiweka  katika  nafasi  hii  kwa  kunipigia  kura  zipatazo  19 dhidi  ya  mpinzani wangu  wa  karibu  Bw.Waziri  Mlenda  ambaye  alikuwa  akitetea  nafasi  hiyo  aliyoitumikia   kwa  mwaka  mmoja  huku  akiambulia  kura  14.


Hii  imenifanya  nijisikie  kuwa nina  deni  kubwa  mbele  ya  madiwani  wa  halmashauri  ya  manispaa  ya  Tabora   na  wananchi  wao kwa  ujumla.


NINASEMA  KWA  KAULI  MOJA  NITAKUWA NAIBU MEYA WA WANANCHI NA SIO  MPIMA VIWANJA NA KUSABABISHA MIGOGORO YA ARDHI,…..”IMEFIKIA  HATUA MHESHIMIWA DIWANI  ANAKUWA  MPIMA  VIWANJA  JAMBO  HILI NI WAPI NA WAPI”…KWA MAANA  HIYO  HATA  DIWANI  UNAJIKUTA  UNAKOSA NAFASI  YA  KUWATETEA  VIZURI  WANANCHI  WALIOKUCHAGUA  UNAKUWA  BIZE  NA  WAPIMA  VIWANJA WENZAKO.....Akacheka kidogo akiashiria kufurahia ushindi wake.


Hivi  ndivyo  nilivyo  msikiliza  Bw.Salumu  Msamazi  muda  mfupi tu  mara  baada  ya  kuchaguliwa  kukiwakilisha  chama  kuwania  nafasi  ya  Unaibu Meya wa  manispaa  ya  Tabora.


Bw.Msamazi  ambaye  katika siku  chache  hizi  za  mchakato  wa kumpata  naibu  Meya  amekumbana  na  changamoto  kadhaa  hata  za  vitisho  dhidi  ya  maisha  yake  lakini hakuvunjika  moyo  kwani  alitambua  kuwa  kila  jambo  la  heri  haliji  kwa  lelemama  bali  lazima  liwe ni  la  mapambano  aidha  kufa  au  kupona.


Si  hivyo  tu  bali  alitambua  kuwa  katika  mapambano  hayo  pia  Sapoti  anayopewa na  washiriika  wake  ikisimamiwa kwa  uweza  mkubwa  wa  Mwenyezimungu  ndio  nguzo  yake  kuu  katika  ushindi  dhidi  dhahma  zote  alizoundiwa  kwa  wakati  huo wote,  kipindi alichokiita  kigumu sana  hata  akaifikiria pia  familia  yake  akaona  JAMII  AU  WANANCHI  NI  BORA  ZAIDI  NA HIVYO  KUPATA  NGUVU  YA  KUENDELEA  NA  MTANANGE HUO  WA  HATARI  LAKINI  SALAMA.


‘’NITASHIRIKIANA  NA  MADIWANI  WENZANGU  NA  NITAKUWA  NA  MSIMAMO  KUTEKELEZA  MAAMUZI  YA  VIKAO  BADALA  YA  MAAMUZI  BINAFSI  KAMA  ALIVYOKUWA  AKIFANYA  ALIYEMALIZA MUDA  WAKE”Alisema  Msamazi.


HABARI  ZILIZOKWEPO  MITAANI.

Vita  hiyo aliyokuwa  akipigwa  Bw.Msamazi  imeelezwa  kuwa  ilikuwa ikihusisha  hata  viongozi wakubwa  wa  CCM  Mkoa  na  baadhi  ya  Wabunge  jambo  ambalo  lilidhihirisha  kuwa  makundi  ni  kitu  kibaya  kabisa  ndani  ya  CCM  na  tena  ni  hatari  kuliko  inavyofikiriwa  sasa.


Eti  inasemekana  kuwa kuna baadhi  ya  wagombea  katika  kinyang’anyiro  hicho waligushi  hata  vyeti  vya  elimu  zao,……Mhmm,..Kwa hili  mie  tena  simo  nawaachia  wanaCCM  wenyewe  ambao  ndio  walikuwa  wakizagaza  hayo  ingawa  kuna  baadhi  ya  vyeti  niliviona  kwa  macho  yangu  lakini  Mhmm,…NISIJE  NIKANG’OLEWA  MENO  NA  KUCHA  KWA  KUTUMIA  PRIZE  KWANI  BADO  NI  MWANDISHI  MCHANGA  SANA  KATIKA  FANI  HII  YA  KUWAJUZA  WATU.

      

No comments:

Post a Comment