Friday, February 1, 2013

BALOZI ATAKA HOSPITAL YA NDALA KUTOA HUDUMA ZA AFYA KWA WATANZANIA


 Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco Padilla Askofu wa jimbo kuu la Tabora Paul Ruzuka akiwa na mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi wakikata utepe wa jengo la kutolea huduma ya mama na mtoto katika hospital ya Ndala baada ya kutimiza miaka 50
 Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco Padilla pamoja viongozi wengine wa serikali ya wilaya ya Nzega  na mtendaji mkuu wa hospital hiyo SR Geogretha Paul aliyeshika sahani ya mkasi na meneja wa kanda wa CSSC SIMIONI KASONGA
Askofu wa jimbo kuu wa tabora Paul Ruzoka akiteta jambo na mwakilishi wa papa hapa nchini

Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco Padilla akipokea zawadi kutoka kwa waumini wa kanisa la parish ya Ndala pembeni yake ni Sr George Paul

Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco Padilla akisoma maji kabla ya kubariki na kuyabariki majengo ambayo haliyafungua







NA LUCAS  RAPHAEL,NZEGA 

Askofu mkuu na balozi wa papa hapa nchini Fracinsco Padilla amesema kuwa nchi ya Vatcan  itafanya kila linalowezekana kuhakikisha hospitali ya ndala wanaisaidiwa ili iweze kutoa huduma za afya kwa  watanzania kwa miaka mingine 50 na kukabiliana na  changamoto zilipo kwa sasa katika hospital zingine.

Kauli hiyo aliitoa baada ya kufungua majengo ya kutolewa huduma kwa mama na watoto pamoja na chumba cha upasuaji chenye  vya  vifaa vya kisasa ambavyo vyote vimegharimu jumla ya shilingi milioni 465

Balozi huyo wa papa hapa nchini alisema kwamba huduma nzuri za afya kwa watanzania ndio kitu muhimu sana kwani bila afya hakuna amani, hakuna upendo na hakuna chochote ambacho wananchi wananweze kupata kumbukumba ya kuwepo kwake hospital hiyo hata baada ya miaka 50 ijayo.

“umati uliofika hapa unataka kujua je huduma zinazotelewa katika hospitali hiyo zitaendelea kuwepo vile vile ama zitakuwa nzuri kwa watu wanaipata huduma hizo “alisema balozi  Padilla

Aidha aliwataka watoa huduma wote wa hospital hiyo kufanya kazi kwa moyo wa kujitolewa kwa watanzania wote wanaofika katika hospital hiyo kupata huduma ya matibabu ili kutumiza malengo ya mungu kwa kutoa na kutoa na kupokea .

Hata hivyo alisema kwamba hospital ya ndala kutimia miaka 50 ikiwa inaendela kutoa tiba kwa wananchi wa Tanzania ni jambo nzuri la kujivunia na lamafanikio makubwa sana kwa kanisa na waumini wake

Awali Sista mkuu wa Hospitali hiyo Bernadette Kessy wakati akisoma risala kwa barozi wa papa nchini Askofu mkuu Fracinsco Padilla kwenye sherehe ya maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 ya utoaji huduma za afya tangu kuanza kwake mnamo mwaka 1963.

Aidha hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki jimbo kuu la Tabora licha ya kutikiza miaka 50 tangu ianze kutoa huduma ya  afya kwa jamii mwaka 1963 bado inakabiliwa uhaba mkubwa wa fedha zakununulia madawa ya kutosha, vifaa tiba, vitendanishi na upungufu wa watumishi wa kada zote.


Kessy alisema kuwa mbali ya ukosefu huo wa fedha pia wanakabiliwa na ukosefu wa chumba cha chenye ukubwa wa kutosha kwa ajili ya kutolea huduma za maabara ya magonjwa ya binadamu.

Pia alisema kwamba hospitali hiyo inaukosefu wa gari la huduma kwa wagonjwa waliombali na hospitali gari ambalo hutumika kusarisha wagonjwa mahututi katika hospitali za rufaa.

Hata hivyo Sista Kessy alimweleza balozi huyo wa Vatcan nchini kuwa pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo lakini wameweza kuboresha miuondombinu ya majengo ya zamani na kuyafanya kuwa ya kisasa .

Aidha amebainisha kwamba mbali na kuboresha majengo hayo, wameeza kujenga majengo mengine manne mpya ambayo ni jengo la huduma ya upasuaji, jingo la huduma ya tiba kwa watu wanaishi na VVU, jengo la huduma ya afya ya mama na mtoto pamoja na jengo la wodi ya wagonjwa wa kifua kikuu.


Mwisho

No comments:

Post a Comment