Sunday, February 17, 2013

WAISLAM NA WAKRISTO WAUNGANE;LOWASSA

 
Na,LUCAS RAPHAEL,,Nzega.
 
WAZIRI Mkuu Mstaafu  Edward Lowassa  amewataka waislam na wakristo wote Nchini kuungana kwa pamoja  kuitetea na kuilinda amani tuliyonayo kwa vitendo.
Akizungumza katika Harambee ya kanisa la Moraviani  kanda ya magharibi iliyofanyika katika wilaya ya nzega mkoani Tabora,kuwa waumini hao kwa pamoja wanapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja katika kuitetea amani iliyopo kwa vitendo.
Lowassa aliendelea kusisitiza kwamba kwa sasa kuna baadhi ya watanzania wanaichezea amani iliyopo kwa sasa hapa nchini na kufanya mauaji ya watumishi wa mungu lakini isiyo Tanzania tunayoihitaji .
Hata hivyo alikuwa na kimwabingizo cha hii ni Tanzania tunayoihitaji ili kuwa na upendo na utulivu amani tunayoisema tutailinda amani kwa nguvu zote hapa Tanzania.
“hii ni Tanzania tunayoitaka kwa waislamu na wakristu kushirikiana katika ibada kama hii leo hapa kanisani “alisema Lowassa.
Alisema kwamba katika maisha yetu ya kila siku ni watu wakutengemeana kwa kila jambo kwani hakuna muda saa ambao uwezi kuacha kumuona muislam akipita njiani na hata mkristo pia katika mitaa nayo ni hivyo hivyo .
Lowassa aliendelea kusisitiza watanzania tunapaswa kuhakikisha kila siku tunamuomba mungu ili kuendeleza amani yetu hapa Tanzania inadumishwa kwa hali na mali.
Hata hivyo katika changizo hilo la harambee ya kanisa la morviani kanda ya magharibi alisema kwamba yeye ni tajiri wa watu nasio tajiri kama watu wanavyosema huko mitaani .
Alisema kwamba watu wanaomsema vibaya kila kukicha waendelea kufanya hivyo kwani kwafanya hivyo wanaendela kumuimarisha kiimani na nguvu kubwa ya ushawishi kwa watu wa mungu amboa ndio wamekuwa wakimuunga mkono kila siku katika kazi ya mungu.
“mimi nitajiri wa watu nasio tajiri wa fedha kama wanavyo sema huko mitaani  na watu wasiokuwa na mapenzi mema na mungu”alisema lowassa
Aidha katika harambee walikuwapo waislamu kutoka mikoa ya mwanza ,shinyanga na Tabora pamoja na viongozi mbalimbali wa siasa kutoka sehemu mbalimbli hapa  nchini.
Askofu Mkuu wa kanisa la moraviani kanda ya magharibi Issack  Nicodemo alisema kuwa waislam na wakristo hapa nchi ni ndugu kutokana na mahusiano yaliyopo toka hapo awali.
Alisema kuwa vitendo vinavyoendelea kufanyika hapa nchini vya mauaji kwa viongozi wa dini ni vyakulaniwa na kongeza kuwa upendo na amani inahitajika kupoteza suala hilo.
Wakati huo huo mbunge wa jimbo la kaliua Profesa Juma kapuya alisema kuwa kunabaadhi ya watu wamelewa na amani iliyopo nchini hivyo amani inapaswa iheshimiwe.
Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm mkoa wa shinyanga Hamis Mgeja aliwataka waislamu na wakristo kuliombea taifa hili ilikuweza kuwa na amani na upendo.
Awali Akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi makamu mwenyekiti wa idara ya wanawake wa kanisa la Morania Agness Nsanto katika harambee hiyo ikiongozwa na waziri mstaafu Edward Lowassa ilifanikiwa kukusanya fedha million 110,168,250,fedha tathilimu zilikuwa Million 36,706,250 wakati ahadi zikiwa Million 71.
Hitaji harisi ilikuwa Millioni 80 ambapo wanawake hao walikuwa na Million 20 kama kianzio cha kukusanya fedha hizo.
Mwisho.
 
 

No comments:

Post a Comment