Wednesday, February 20, 2013

MWANAFUNZI AJINYONGA KWA MATOKEO MABAYA YA KIDATO CHA NNE MWAKA HUU



 Na Lucas Raphael,Tabora


Siku chache baada ya matokeo ya kidato cha nne kutangazwa nchini  mkoani tabora mwananfunzi  aliyemaliza kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Kanyenye mjini Tabora, amejinyonga kufuatia matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka huu.

akizungumza na waandishi wahabari ofisini kwake kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora  ACP Anthony Rutta amemtaja mwanafuzi huyo kuwa ni Michael Fidelis (19) ambaye ni mkazi wa skanda mtaa Mwinyi kata ya chemchem Manispaa ya Tabora.

Alisema mwanafuzi huyo alienda kuangalia matiokeo ya kidato cha nne majira ya saaa 11 jioni Februari 18 mwaka huu na badaye kukutwa amejinyonga hadi kufa chumbani kwake kwa kutumia kamba ya manila.

Kamanda Rutta alieleza kuwa marehemu alipata darajala mwisho kwa maana ya sifuri aliacha ujumbe uliosomeka “Nisamehe sana mama usitafute mchawi, nakupenda sana, uwamuzi niliochukua nisababu ya matokeo mabaya, nakutakia maisha mema” ulisema sehemu ya ujumbe huo.

Mkuu wa shule ya sekondari ya kenyenye alipokuwa akisoma mwanafunzi Fidelis, Kapufi Patson alisema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ni mpole na mtaratibu na wameshangazwa na uwamuzi aliochukua wa kujinyonga.

Matokeo ya shule ya sekondari ya mwinyi yanaonyesha hakuna mwanafuzi aliyepata alama ya ya kwanza na  yapili huku waliopata darajala tatu wakiwa wanafuzi wawili, daraja la nne 14 na waliopata sifuri ni wakiwa wanafunzi 85, wakati wanafuzi 36 matokeo yao hayaktoka kwasababu walikuwa wanadaiwa ada ya mtihani.

 Mwisho

No comments:

Post a Comment