Wednesday, February 6, 2013

NMB YAFADHILI MKUTANO MKUU WA WANAHISA WA CHAMA CHA MAWAKALA WA FORODHA TANZANIA (TAFFA)

Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam Salie Mlay akieleza umuhimu wa makampuni ya mawakala wa forodha kuwa na akaunti na benki wakati wa hafla ya mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki jjijini Dar esaalam Benki ya NMB ikiwa ndio mdhamini katika hafla hiyo.
Sehemu ya wanachama wa chama cha mawakala wa forodha Tanzania na maofisa wa NMB waliohudhuria mkutano mkuu wa chama hicho. NMB wakiwa ndio wadhamini wa mkutano huo.Ambapo wanachama hawa waliweza kufungua akaunti kwa ajiri ya kampuni zao.makampuni yapatayo 60 yaliweza kufungua akaunti siku hiyo.
Meneja mahusiano na huduma za kibiashara za kibenki wa NMB Noelina Kivaria akimtambulisha Meneja masoko wa NMB Shilla Senkoro kwa Rais Mstaafu wa chama cha mawakala wa forodha Tanzania ndugu O.O.Igogo mara tu baada ya mkutano huo mkuu wa wanachama wa chama cha mawakala wa forodha Tanzania

Mwishoni mwa wiki NMB ilifadhili mkutano mkuu wa Wanachama wa chama cha mawakala wa forodha ambao ulifanyika jijini Dar es salaam na hii ni kutokana na ukweli kwamba NMB ndio benki pekee yenye matawi 147 ambayo yameenea nchi nzima. Katika kuhakikisha huduma bora kwa wateja wake na inao mkakati wakuwafikia wateja wake katika ngazi ya vijiji.

Chama cha mawakala wa forodha Tanzania ni moja kati ya wateja wakubwa wa NMB na wanachama hawa wamesambaa nchi nzima hivyo benki pekee ambayo inayoweza kuwasadia katika shughuri zake za kila siku ni NMB pekee.NMB kwa kuanzisha na kuendelea kua na mahusiano mazuri na wateja wake imeweza kutoa ushirikiano huo mzuri kwa chama hiki cha mawakala wa forodha Tanzania mwishoni mwa wiki kwa kutoa udhamini katika hafla yao

No comments:

Post a Comment