Monday, February 4, 2013

MADIWANI KUKIONA CHA MOTO CCM

 
Na Lucas Raphael,Nzega

 

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) Mkoani Tabora kimesema madiwani ambao hawakuhudhuria katika sherehe za maadhimisho ya chama hicho kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu kutokana na kutoheshemu sherehe hizo .

Hayo yalisemwa na katibu wa chama hicho mkoa  wa Tabora Iddi Ame katika sherehe za maadhimisho ya kuzaliwa kwa chama hicho kimkoa zilifanyika wilayani Nzega ambapo kwa sasa kina sherehekea miaka 36 toka kizaliwe.

Alisema kuwa kuwa baadhi ya madiwani kupitia tiketi ya chama hicho hawakuhudhuria katika sherehe za maadhimisho ya kuzaliwa kwa chama mapinduzi CCM wahesabu wameumia kwa kitendo chao hicho.

Alisema kuwa kitendo hicho chakuto kuhudhuria sherehe hizo kubwa za kitaifa ni kukiuka maadili ya chama hicho na chadharau kwa chama hicho.

Aliwataka madiwani hao pamoja na viongozi wengine wa kichama kuheshemu sherehe hizo muhimu za kitaifa pamoja na maagizo mbalimbali ya chama.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho mkoani hapa ,Hassani Wakasuvi aliwata viongozi hao kuweka utamaduni wa kuzungumza na wananchi mara kwa mara ilikujua kero zao na kuzifanyia utatuzi mapema.

Alisema kuwa viongozi hao endapo wakizungumza na wananchi kwa nyakati mbalimbali wataweza kujiwekea imani kwa wananchi hao kwa kutatua matatizo yatokeapo kwenye maeneo yao .

Mwenyekitu huyo aliwataka wabunge wa mkoa wa Tabora kushirikiana kwa kikamilifu katika katika kutetea hoja zenye maslahi ya wananchi ili kutimiza ahadi zao walizokuwa wamewaahidi wananchi hao wakati walipokuwa na wanaomba uwakilishi bungeni.

Mwisho.
 

No comments:

Post a Comment