Monday, February 4, 2013

"WAZEE WABARIKI NDOA KANISA LA MORAVIAN TABORA,WENGI WAFURAHIA TUKIO LA KIHISTORIA"

 Mchungaji akiwaaga wanandoa baada ya Ibada takatifu ya kubariki ndoa hiyo katika kanisa la Moravian Tabora ambapo Mzee Laurent Mchele alibariki ndoa yake na mkwewe Bi.Devota Laurent Mrisho.
Mchungaji akitoa mawaidha kwa ajili ya kuwaasa wanandoa Mzee Laurent Mchele na mkewe Bibi.Devota Laurent Mrisho wakati wa kubariki ndoa hiyo iliyokuwa kivutio kikubwa kwa waumini waliohudhuria katika ibada kanisa la Moravian Tabora mjini.

 Wakati wa kubariki ndoa hiyo huku mamia ya waumini wakishuhudia tukio hilo la heri kwa wanandoa hawa wawili.
 Wanandoa baada ya ibada ya kubariki ndoa hiyo wakiwa wametulia kama ilivyozoeleka kwa maharusi.


Mara baada ya kubariki ndoa hiyo baadhi ya ndugu na jamaa wa karibu pamoja na watoto, wajukuu wa Mzee Laurent Mchele na mkewe Bibi.Devota Laurent Mrisho walipiga picha ya pamoja ikiwa ni kumbukumbu ya tukio hilo la kihistoria.

No comments:

Post a Comment