Monday, February 4, 2013

WATAKA BIMA YA AFYA IBORESHWE




 
 Na Lucas Raphael,Nzega

WANACHAMA  wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Wilayani Nzega  Mkoani Tabora  wameutaka mfuko huo uboresha huduma zake katika Hospital ya wilaya ya Nzega  ili wachama wa mfuko waweze kunufaika na huduma hizo
 
Wakizungumza katika kikao cha Bima ya Afya kilichoandaliwa na Bima ya AFya kanda ya Magharibi,walisema kuwa katika hospitali ya Nzega kuna uhaba mkub wa wa Dawa hali ambayo wananchama  huwapelekea kununua katika maduka ya Dawa nje ya hospital hiyo .
 
Licha ya kutokuwa na Dawa katika Hospitali  ya wilaya,wanachama hao wameiomba Bima ya Afya kanda ya magharibi kupitisha moja ya Duka la Dawa muhimu ambalo litakalo weza kuwasaidia wanachama hao, wakosapo Dawa katika Hospitali ya wilaya .
 
Walisema kuwa Duka la Dawa litakapo patikana wilayani hapa pamoja na maduka mengine vijijini yataweza kuondoa kero na madukuduku ya wanachama hao hasa wakosapo huduma katika hospitali ya wilaya.
 
Wakitoa malalamiko yao walisema kuwa baadhi ya watoa huduma hospitalini hapo hutumia lugha chafu kwa wanachama hao pamoja na kutozwa pesa kwa gharama ya matibabu watakayo patiwa.
 
Wakitoa ushauri wameutaka mfuko huo wa Taifa wa Bima ya Afya  kuboresha huduma bora za Afya pamoja na kufuata sera za mfuko huo ili wanachama wanufaike maradufu.
 
Kaimu Meneja kanda ya Magharibi, Hipolit Lello alikiri kuwepo kwa uhaba wa Dawa katika Hospital ya wilaya ya Nzega pamoja na zahanati zake.
 
Lello akitoa ushauri kwa Halmashauri ya wilaya kuwa itume maombi ya kupata fedha za tele kwa tele zitakazo weza kununua Dawa pamoja na kuboresha mazingira ya huduma bora kwa wananchama hao tofauti na sasa wanavyo lalamika.
 
Aliwataka wanachama hao kuwa hamasisha wadau wengine wajiunge katika mfuko huo lengo likiwa ni kuwa saidia katika huduma za Afya zenye bei nafuu pamoja na kuwa himiza wananchi kujiunga na (CHF), ambapo  kaya  zilizo andikishwa  8,245 sawa na  7% ya kaya zote.
 
Alisema kuwa kwa Idadi hiyo ni kidogo tofauti na matarajio ya zoezi hilo ambalo ni mmoja ya huduma zenye gharama nafuu kwa watumishi pamoja na wananchi kwa ujumla.
 
MWISHO.


No comments:

Post a Comment