Monday, February 4, 2013

MAAFISA HABARI WA SERIKALI WAPIGWA MSASA MKOANI DODOMA

Picha na 1Waziri wa Habari, Vijana ,UtamaduninaMichezoDkt. Fenella Mukangara akifungua mkutano wa maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali mjini Dodoma. Pamoja na mambo mengine amewataka kufanya kazi   kwa kuzingatia weledi na kutoa taarifa sahihi kwa umma mara kwa mara kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali.
Picha na 2Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja naWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi hicho  mjini Dodoma.
Picha na 3Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa Kikao kazi hicho mjini Dodoma.
Picha na 4Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwasilisha mada kuhusu Mtazamo mpya wa Mawasiliano katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma.
Picha na 5Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali  Sarah Reuben akichangia moja ya mada katika kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma.
Picha na 7Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi chao kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi Mjini Dodoma.
Picha no 6Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi chao kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi Mjini Dodoma.
Picha no 8Mmiliki na muendeshaji wa mtandao wahabari na matukio wa Mjengwa Blog kutoka Iringa Bw. Majjid Mjengwa akitoa mada kwa maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali kuhusu Faida na Changamoto za matumizi ya mitandao ya kijamii kwa mawasiliano  serikalini mjini Dodoma.PICHA NA ARON MSIGWA WA MAELEZO

No comments:

Post a Comment