Thursday, June 20, 2013

MAJAJI MAHAKIMU WALALAMIKO KANDA YA MAGHARIBI



Na Lucas Raphael,Tabora




JUMLA  ya malalamiko 36 yalipokelewa na ofisi ya  maadili  kanda ya magharibi katika kapindi cha mwanka jana na mwaka huu kwa maafisa wa mahakama kwa kuchelewesha kesi na kupokea rushwa kwa lengo la kupendelea hukumu.

Maelezo hayo yalitolewa na kamishna wa sekretarieti ya maadili ya viongozi jaji mstahafu Salome Kaganda alipokuwa akimkaribisha mkuu wa mkoa wa tabora Fatma Mwassa wakati wa  kufungua mafunzo kwa mahakimu katika ukumbi wa mtemi Isike mwanakiyungi mkoani tabora jana .

Alisema kwamba katika malalamiko hayo 15 sawa na asilimia 41 .6 ni malalamiko  kwa maafisa wa mahakama ,wakiwepo majaji na mahakimu wa ngazi mbalimbali kwa kuchelewesha kesi na kupokea rushwa .

Jaji Kaganda aliendelea kusema kwamba idara ya mahamaka ni miongoni mwa  Idara za serikali zinazolalamikiwa sana kwa vitendo vya Rushwa ,kutokutenda haki na kukosekana kwa uadilifu.

Alisema kwamba mafunzo hayo lengo lake ni kuwajengea uwezo viongozi wa katika kuifahamu na kuitekeleza sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995 ambayo ndio sheria mama inayosimamia maadili ya viongozi wa umma nchini.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa tabora Fatma Mwassa akifungua mafunzo hayo katika hotuba yake iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya Tabora Sulemani Kumchaya alisema kwamba utumishi wa umma kwa ujumla bado una matataizo na mapungufu mengi ya kimaadili ,utoaji wa huduma usioridhisha ,migongano ya maslahi matumizi mbaya ya madaraka hivyo vyote ni changamoto inayowakabilia watumishi walio wengi hapa nchini .

Alisema kwamba mafunzo haya yawe ni chachu ya mabadiliko kwa kada ya mahakimu mkoai hapa kwa kufanya kazi kwa kufuata maadili kanuni sheria na busara .

“hali hiiitakuza matumaini na imani ya wananchi kwa serikali na hususani mhimili wa mahakama kama chombo kikuu cha kusimamia haki kwa umma”alisema mwassa.

Mafunzo hayo yaklioandaliwa na ofisi ya maadili ya viongozi kwa mahakimu kwa wafawidhimkoa na wilaya na wale wa mahakama za mwanzo kutoka katika wilaya saba za mkoa wa  tabora .

Mwisho

No comments:

Post a Comment