Monday, June 17, 2013

MUNDE AWAKOMBOA MAKATIBU U.W.T TABORA MJINI,ATOA MSAADA WA BAISKELI ZENYE THAMANI YA SH.MIL.3.75

Baadhi ya Makatibu kata wa U.W.T Tabora mjini wakijitayarisha kuondoka baada ya kukabidhiwa baiskeli zao kama chombo cha Usafiri watakachokitumia kuzunguukia wanachama wao ikiwa ni mkakati wa kukiimarisha CCM kupitia Jumuiya hiyo ya Umoja wa Wanawake ambapo baiskeli hizo zimetolewa na Mbunge wa Vitimaalum Mh.Munde Tambwe.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora manispaa Bw.Moshi Abraham maarufu Nkokota akikabidhi msaada wa baiskeli 25 aina ya Phoniex zenye thamani ya shilingi mil.3,750,000/=kwa makatibu kata wa UWT zilizotolewa na  Mbunge wa vitimaalum  mkoa wa Tabora Mh.Munde Tambwe kwa ajili ya kurahisisha shughuli za Jumuiya hiyo ya UWT.



No comments:

Post a Comment