Sunday, June 30, 2013

TFDA YATEKETEZA ZAIDI YA TANI 2 ZA VIPODOZI TABORA

 

Mkaguzi wa Mamlaka ya Chakula na dawa TFDA kanda ya Kati na Magharbi Bw.Aberl Deule akifumua baadhi ya vipodozi kwa ajili ya matayarisho ya kuteketeza kwa moto zoezi linaloendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Tabora.    
 
 NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
 
MAMLAKA ya chakula na dawa nchini (TFDA), kanda ya magharibi na kati,imeteketeza bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu, zenye thamani ya sh milioni 3.2.
Zoezi la kuteketeza bidhaa hizo lilifanyika mkoani Tabora baada ya kufanyika ukaguzi maalumu kwa wiki mbili kwenye maduka,majengo,Phamacy bohari ya dawa na maeneo mengine muhimu.
Akizungumza na waandishi wa habari eneo la kuteketeza bidhaa hizo,mkaguzi kanda ya kati na magharibi,Abel Deule,alisema ukaguzi huo ulihusisha watalaam toka ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Tabora na halmashauri ya manispaa Tabora na ukaguzi huo ulihusisha biashara ya chakula,dawa,vipodozi na vifaa tiba.
Deule aliongeza jumla ya majengo 192 yalikaguliwa na ambapo lengo lake ni kuangalia majengo hayo,usafi,hali ya usajili na vibali toka mamlaka ya chakula na dawa,(TFDA),hali ya ubora wa bidhaa za chakula,dawa,vipodozi, vifaa tibauwepo vifaa bandia zenye viwango duni na uwepo vipodozi vyenye viambata vyenye sumu.
Aidha Deule alisisitiza kutokana na ukaguzi huo,licha wafanyabiashara hao kuwa na uelewa,bado wamekuwa wakiuza vipodozi vyenye viambata vyenye sumu vilivyozuiliwa kuuzwa na ktumika nchini kwa mujibu wa kifungu namba 88 (a) cha sheria ya chakula, dawa na vipodozi namba 1 ya mwaka 2003.
Alisema bidhaa zilizokamatwa na kuteketezwa ni bidhaa za chakula tani 0.129 ya thamani ya sh 775,000,bidhaa za vipodozi zilizoisha muda wa matumizi na zenye viambato vyenye sumu tani 0.245 vya thamani y ash sh milioni 2,298,400 na dawa za binadamu tani 0.001 zenye thamani ya sh 158,000.
Aidha aliongeza kwenye ukaguzi huo pia kulikutwa maziwa ya watoto ,Lactogen namba 1 na 2 na NAN ambayo ni bandia, dawa ya chanjo ya mifugo ya Newcastle (1-2) iliyositishwa kuuzwa,dawa bandia aina ya Doxycycline Capsules gramu 100,pombe kali iitwayo Shujaa gin ambayo haijapata usajili toka mamlaka ya chakula na dawa.
“Kutokana na hali hiyo tumechukua hatua za maduka yaliyokutwa na vipodozi vyenye viambata vya sumu….. wamiliki walilipa ada ya vibalivya kuteketeza,wateja ambao majengo ambayo hayajapata usajiliwalijaza fomu na kulipia ada kwa vibali husika ikiwemo duka moja kufungwa kutokana na mmiliki kuwa mkaidi kwa maafisa.” alisema Deule.
Aliongeza hata hivyo wakati wa ukaguzi wafanyabiashara walielimishwa kuhusu bidhaaza vyakula,dawa.vipodozi,ikijumuishwa bidhaa za vipodozi zenye viambato vyenye sumu,na bidhaa duni na bandia ya chakula (Lactogen 1/2 na NAN 1/2.

No comments:

Post a Comment