Thursday, June 20, 2013

MWANAMKE ANA NAFASI KUBWA YA KUCHANGIA MAENDELEO


 NA LUCAS RAPHAEL,TABORA


IMEELEZWA KUWA Suala la kijinsia halina budi kupokelewa ili kumpa nafasi mwanamke yakuweza kuchangia maendeleo ya familia na taifa kwa ujumla .

Kauli hiyo ilitolewa na mmoja ya wakazi wa kijiji cha Kigwa AZIZA RAMADHANI wakati akichangia mdahalo wa Mwanaume na mwanamke.

Kauli hiyo, waliitoa jana kijijini hapo kwenye mdahalo  wa usawa wa kijinsia na maendeleo, ulioandaliwa na Shirika la mtandao wa mandeleo ya jamii wilayani Uyui (UCODEN) kwa ufadhiri wa The Foundation for Civil Society kutoka Dar es Slaam.

Alisema kwamba mwanaume na wananmke washauriane katika shughuli mbalimbali ili kujiletea maendeleo.

“Mwanaume asijione kuwa yeye ndiyo binadamu na mwanamke ni mashine ya kufanya kazi katika jamii.alisema AZIZA

Alisema kwamba kila mtu ana sehemu yake katika kuleta maendeleo katika jamii.Tatizo ni kina baba kujiona kuwa wapo juu kuliko mwanamke bila kujali uwezo alio nao mwanamke.

Alisema kuwa baba pekee yake hawezi kuleta maendeleo ni lazima kuwepo na mchango wa mwanamke.


Amina Christopher Mjema:naye alisema kuwa  wazazi wengi wananchangia mtoto wa kike kushindwa kufanya vizuri katika elimu kutokana na tabia ya wazazi kuhamasisha watoto wao wa kike kuolewa badala ya kuhamasisha watoto hao kusoma zaidi.

Hata hivyo Diwani wa kata ya Kigwa Katyavi Salumu alisema kwamba kuna na changamoto nyingi katika masuala ya kijinsia mfano kipigo kwa kina mama limekuwa tatazi kubwa kwa jamii yetu.

Alisema kwamba mgawanyo hafifu wa mali,hii inatokana na kurithi tabia kutoka kwa mababu bila kuangalia athari za mila hizo za mababu.

Aliongeza kusema kwamba pia kina mama wanajirudisha nyuma kutokana na kushindwa kwao kutoa maamuzi ya jambo fulani na badala yake wamekuwa wakiwasubiri waume zao.

Kwa upande wa elimu, diwani huyo alisema watoto wa kike nao wamekuwa wakichangia katika kuwanyima fursa ya elimu kutokana na mabadiliko ya ukuaji ni vema jamii kuangalia kwa makini kuhusu malezi ya vijana.

Hata hivyo Mratibu wa UCODEN Christopher Nyamwanji aliwashukuru sana washiriki kwa maoni yao ambayo yameonesha uzoefu wa masuala ya kijinsia katika kata ya Kigwa na pia aliwasihi wakazi wa Kigwa kujitokeza tena siku nyingine katika shughuli kama hii.

MWISHO

No comments:

Post a Comment