Tuesday, June 11, 2013

POLISI TABORA WAKAMATA BANGI YENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.68

 
 

 NA LUCAS RAPAHEL,TABORA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora  ACP Peter Ouma akiangalia magunia ya bangi yaliyokamata Wilayani Nzega ambayo yalikuwa yakisafirishwa,mzigo huu ulikuwa na thamani ya zaidi ya shilingi mil.68.


 

JESHI la Polis wilayani Nzega mkoani Tabora linawashikilia watu wa 4nne kwa tuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya bangi zaidi ya gunia sita 6sawa la kilo 168 zikisafirishwa kuelekea mkoani Shinyanga zikiiwa na thamani ya shilingi milioni 68.7.
 
Akizungumza na waandishi wa Habari kamanda wa polis mkoani Tabora Peter Ouma alisema kuwa Tukio hilo limetokea June 6 mwaka huu  katika kijiji cha kilabili kata ya Nata wilayani hapa majira ya saa tatu asubuhi.
 
Alisema kuwa Jeshi hilo lilipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna watu wanapitisha madawa hayo aina ya bangi.
 
Alisema kuwa kwa kupata taarifa hizo kutoka kwa wananchi wema Jeshi hilo liliweka mtego mkari ambapo ulifanikisha kuwa nasa wahari hao wakiwa na madawa hayo aina ya bangi magunia sita (6).
 
Alisema kuwa wahalifu hao wakiwa wamebeba bangi hizo kwenye baiskeli kila mmoja magunia mawili mawili wakitokea kijiji cha ugembe nzega kuelekea Manonga tinde mkoani shinyanga.
 
Kamanda Ouma aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Paul Batoni (41)mkazi wa manonga tinde shinyanga,Kashindye Seleli(21) mkazi wa manonga Tinde shinyanga,Shaya kapaya(20)mkazi wa manonga tinde shinyanga pamoja na Moshi Joseph (22)mkazi wa Ugembe puge shinyanga.
 
Alisema kuwa Jeshi la polis linaendelea kuwashikilia watuhumiwa hao kwa mahojiano zaidi ilikupata mtandao huo wa usambazaji wa madawa hayo ya kulevya aina ya bangi na kuongeza kuwa pindi upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahamani kujibu tuhuma hizo zitakazo wakabili.
 
Mwisho.


No comments:

Post a Comment