Thursday, July 18, 2013

GARI LA ABIRIA, AIRBUS LIFANYALO SAFARI ZAKE TABORA NA DAR LAPATA AJALI ENEO LA MASEYU-MOROGORO

 
 
Basi la Airbus likiwa limeacha njia.

ABIRIA 23 waliokuwa wakisafiri na basi la Air Bus linalofanya safari zake kati ya Tabora na Dar wamejeruhiwa, na wanne kati yao wamejeruhiwa vibaya baada ya basi hilo kupinduka eneo la Maseyu, mjini Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotangazwa na Radio One ni kwamba basi hilo lilipinduka kutokana na mwendo kasi wakati likijaribu kuyapita malori na kupoteza muelekeo kabla ya kupinduka.

Taarifa hizo zinasema kuwa, majeruhi wameumia vibaya maeneo ya kichwani, kifuani na miguuni na wamekimbizwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro, huku wanne akiwemo dereva wa basi hilo wenyewe wakiwahishwa jijini Dar es Salaam katika hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kati ya abiria hao waliojeruhiwa 13 wamelazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro.

taarifa zaidi zinaendelea kufuatiliwa ili kujua kinachoendelea, ingawa mpaka sasa hakuna kifo chochote kilichoripotiwa.

No comments:

Post a Comment