Saturday, July 13, 2013

YALIYOJIRI TABORA NDIO KWETU LEO HII,"CCM TABORA MJINI WAANZA BALAA"

RAGE AMSHITAKI MWAKASAKA MAKAO MAKUU CCM TAIFA! Ndg wana TNK, habari nilizozipata muda si mrefu zinadai kuwa Mbunge wa jimbo la Tabora Bwana Ismail Aden Rage amemshitaki Ndg Mwakasaka makao makuu ya ccm Taifa kwa hoja kuwa ameanza kampeni kabla ya muda wake, aidha bwana Mwakasaka ambaye pia aliwahi kuwa mhasibu wa NCCR mageuzi mkoa wa Tabora kwa madai ya Bwana Rage amekuwa akihonga vijana bia na soda kiasi vijana wengi wa Tabora kuchanganyikiwa hasa siku za Dansi na Disco Orion, na katika hali ya sintofahamu Rage amedai kuwa Mwakasaka amekuwa akitumia nguvu ya ziada kulazimisha vijana wamuunge mkono hali iliyopelekea kugombana na Mc Muhina(Diwani wa kitete) ambapo Rage anadai Mwakasaka alimfata Bwana Muhina Chooni Orion na kumpiga Ngumi kwa tofauti za kisiasa nimejaribu kumtafuta Bwana Daniel Muhina juu ya sakata hilo amegoma kata kata kuongelea lolote na kusema yeye kwa sasa ni mtendaji wa CCM asingependa kujiingiza huko na kudai kama Rage anao ushahidi huo aulizwe yeye Rage na si Bwana Muhina.
Like · · Follow Post · · 6 hours ago

No comments:

Post a Comment