Tuesday, July 16, 2013

POLISI TABORA YADAI KUMKAMATA MKULIMA NA RISASI 60 ZA SMG


Kamanda wa  Polisi  mkoa  wa  Tabora  ACP Peter  Ouma  akionesha  risasi za  bunduki aina  ya  SMG ambazo  wamezikamata  barabara  ya  Sikonge  Manispaa ya  Tabora,ambapo Jeshi hilo la Polisi  linamshikilia  Robert Maziku(40) mkulima mkazi wa Mwanzaroad  Tabora mjini. 
Risasi  60 zilizokamatwa kwa Robert Maziku mkazi wa Mwanzaroad Tabora mjini.

Na Lucas Raphael,Tabora

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Robert Maziku(40) mkazi  wa Mwanzaroad manispaa ya Tabora kwa tuhuma za kumkuta na risasi 60 za bunduki aina ya SMG isivyo halali.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Peter Ouma aliueleza mtandao huu  kuwa kukamatwa kwa  risasi hizo ni matokeo  ya  msako  wa mara  kwa  mara  unaofanywa  na Jeshi  hilo  kupambana  na vitendo  vya  kiharifu  katika  maeneo  mbalimbali ya  mkoa  wa  Tabora.

Alisema  mnamo  tarehe  5/7/2013 majira ya saa  nane  usiku huko  barabara  ya  Sikonge  manispaa  ya  Tabora,Robert Maziku  alikamatwa na risasi  hizo  alizokuwa amezihfadhi kwenye kibegi kidogo cha mgongoni  akiwa anataraji kuzipeleka kusikojulikana  kwa  ajili  ya  kufanyia  uharifu.

Kamanda  Ouma  ambaye alitamba  tayari  mtuhumiwa huyo Maziku amekwisha fahamisha Polisi  mahala  ambako Bunduki wanayoitumia wameihifadhi yeye na wenzake ambao hata hivyo hakutaka  kutaja majina yao.

Aidha  sambamba  na kukamatwa kwa risasi hizo Ouma  alisema Jeshi  hilo  wamekamata silaha aina  ya Shortgun  yenye nambari 00NN094188 ikiwa imetelekezwa shambani  katika kijiji cha Busodi wilayani Kaliua baada ya msako mkali uliojumuisha  askari Polisi na wananchi.

Katika wilaya ya Urambo  zoezi  la  msako huo  mkali ulifanikiwa kumtia nguvuni  Katondo Paul(49)mkazi wa kijiji  cha Mirambo tarafa ya Ussoke akiwa anamiliki silaha aina ya Gobore 1,vipande vya gololi 28,baruti kilo 5,watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani hivi  karibuni.        

No comments:

Post a Comment