Saturday, July 13, 2013

WATOTO WARUNDI WALIOSALIMIKA KUUZWA WALIPATA HIFADHI IDARA YA UHAMIAJI TABORA


Watoto ambao ni raia wa Burundi na Rwanda waliokuwa wakisafirishwa kwa lengo la kutaka kuuzwa ili wakatumikishwe kwenye mashamba ya tumbaku walipata hifadhi ya Malazi na Chakula kutoka kwa maafisa wa Idara ya Uhamiaji Tabora,ambapo maafisa hawa walikuwa wakichangishana fedha wao kwa wao kwa ajili ya kuwanunulia Chakula watoto hawa ambao kwa upande wa huduma za malazi walikuwa wakilala katika moja ya ofisi za Idara hiyo hapa mkoani Tabora.

No comments:

Post a Comment