Friday, July 5, 2013

MLOKOLE AMTUFYA MAGUMI MKEWE KWA KUKATA KUENDESHWA KUPANDA BAISKELI NA MTU ALIYELEWA TABORA


Mwanamke huyo (pichani) ambaye jina lake halikufahamika mara moja ameambilia kichapo huku jua likiwaka.
Njemba ambayo ilijitahidi sana kufichama mara baada ya kukumbana na jicho la kamera la mtandao huu alionekana mwenye ujasiri wa kumdharirisha mkewe mbele za watu
(wadaiwa kuwa ni walokole wakristu wa kanisa la Pentekoste)
 
WAKAZI WA MTAA WA KANYENYE-TABORA WAKISHUHUDIA NJEMBA IKIFOKA KANA KWAMBA HAONI KAMA SI VIZURI KWA KITENDO ALICHOFANYA
 
Njemba hiyoooooo ikiongoza kusepa kuelekea nyumbani baada ya soo hilo kukatika......
-------------------------------------
WANANDOA HAO AMBAO WAMEDUMU KWENYE NDOA KWA MIAKA MITATU (3) LEO WAMEJIKUTA WAKITIWA KATIKA TUKIO LA UNYANYASWAJI NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA PALE MME ALIPOKUWA AKIMBURUZA MKEWE KWA NGUMI NA KUMDONDOSHA MARA KADHAA MKEWE HUYO KATIKA BAISKELI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA.

CHANZO CHA UGOMVI
Ni pale mwanaume alipomtaka humbeba mkewe katika chombo chao cha usafiri kupitia barabara kuu ya lami huku akiwa amelewa, ikiwa si kawaida yake mwanume huyo ambaye ndo siku tu ya kwanza analewa na kusababisha yote hayo ndipo mwanaume alihisi kudharauliwa na mkewe.

SABABU ZA MWANAMKE KUKATAA KUPANDA BAISKELI
Mwanamke huyo aliyekuwa amechoka kwa uchovu wa kuumwa akiwa na tatizo la PRESHA YA KUPANDA, huku akiwa anaendelea katika matumizi ya dozi hiyo haikuwa rahisi kwa mgponjwa huyo kuchukuliwa katika baiskeli.

No comments:

Post a Comment