Wednesday, July 24, 2013

MAOFISA WA TATU WA KAMPUNI YA CCCC WAFIKISHWA MAHAKAMANI

WACHINA WAKITIKA KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI WILAYA YA NZEGA KUJIBU MASHTAKA YA KUPIGA NA KUJERUHI WAFANYAKAZI WAO
 
 
RAIA WA WAKICHINA WAKISHUKA KWEYE MAGARI YAO KATIKA VIWANJWA VYA MAHAKANAI WILAYA YA NZEGA MKOANI TABORA


NA LUCAS RAPHAEL NZEGA

MAOFISA wa Tatu wa kampuni ya Chanines  Communication and Construction Campany(CCCC) inayohusika na ujenzi wa barabara kutoka nzega hadi Tabora, wenye athiri ya bara la Asia wamefikishwa katika mahakama ya Hakim mkazi wilaya ya Nzega kwa tuhuma za kuwapiga walinzi watatu na kuwajeruhi vibaya.

Mapema jana katika mahakama hiyo waendesha mashitaka wa Jeshi la polis wilaya wakiongozwa na Inspector Fadhili mpimbwe wameiambia mahakama hiyo kuwa watuhumiwa watatu wa kampuni ya CCCC wanatuhumiwa kwa makosa ya kupiga na kujeruhi.

Mpimbwe aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Afisa Utawala wa kampuni hiyo Long Quan(28) mkazi wa Itilo raia wa china, Fundi wa magari Wang Dong Liang(35)mkazi wa Itilo raia wa china Pamoja na Afisa  Usalama Zhang Han Pang(37) mkazi wa itilo raia wa china.

Mwendesha mashita aliiambia mahakama hiyo mbele ya Hakim mkazi Slvester Kainda kuwa manamo July 21 mwaka huu majira saa saba usiku katika kijiji cha Mwanhala watuhumiwa hao waliwapiga na kuwajeruhi vibaya walinzi watatu wa kampuni hiyo ya ujezni ya CCCC na kuongeza kuwa upelelezi bado unaendelea.

Mpimbwe aliwataja walinzi hao waliopigwa na maofisa wa kampuni hiyo kuwa ni Juma sira,Martin Marco pamoja na Samweli Kuli wote wakiwa wafanya kazi wa kampuni hiyo ya ujenzi katika Idara ya ulinzi,ambapo majeruhi wawili wamelazwa katika Hosptal ya wilaya ya Nzega huku majeruhi mmoja akiwa amelazwa katika Hospital ya Rufaa ya Nkinga wilayani Igunga.

Watuhumiwa hao wamekana kuhusika na tuhuma hizo za kuwa piga na kujeruhi walinzi wa kampuni hiyo.

Mahakama hiyo imetoa uhuru wa dhamana kwa watuhumiwa hao huku ikitoa masharti matatu ya kuzingatia katika dhamana hiyo kuwa ni kila mtuhumiwa kupata mtu mmoja na pesa Tsh,1,000,000, kuwasilisha hati za kusafiria zote pamoja na kutosafiri nje ya wilaya ya Nzega mpaka kibali maalum cha mahakama.

Mahakama hiyo imeahilisha shauri hilo hadi mwezi july 30 mwaka huu itakapo anza kusikilizwa.


Aidha Baadhi ya wananchi waliokuwa nje ya mahakama hiyo wameilalamikia kampuni hiyo ya ujenzi CCCC kutoka China kwa kuwapiga wafanya kazi wake mara kwa mara pamoja na kutokuwa na mahusiano bora na wananchi.

Mjumbe wa serikali ya kijiji cha Mwanhala aliyejitambulisha kwa Juma hamis Selemani ameiomba serikali iingilie kati kuhakikisha mahusiano bora ya wananchi na wakandarasi hao yanaongezeka.

Mwisho.



No comments:

Post a Comment