Wednesday, July 24, 2013

MAKAMANDA WA CHADEMA WAFIKISHWA MAHAKAMA KUU KANDA YA TABORA


Makamanda wa Chadema wanaokabiliwa na kesi ya Ugaidi wakiingizwa Mahakama kuu  Tanzania kanda ya Tabora  kwa mara ya kwanza,aliyevaa  gwanda nyeusi ni kiongozi wao ambaye ni kaimu katibu wa Chadema mkoa wa Dar-es-salaam Bw.Henry Kilewo.

 Joyce Kiria mke wa Bw.Kilewo akiwa na baadhi ya makamanda wa Chadema ndani ya ukumbi wa Mahakama kuu kanda ya Tabora wakisubiri kuanza kwa mahakama hiyo.
Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo makamanda walipakizwa ndani ya gari tayari kwa kurejeshwa mahabusu Gereza la Uyui mkoa wa Tabora.

NA LUCAS RAPHAEL,TABORA

Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Tabora imeahirisha usikilizwaji wa shauri la jinai linalowakabili wanachama watao wa Chama cha Demokrasia na Maendelo – CHADEMA – hadi tarehe 30 mwezi huu baada ya kutokea ubishani hoja za kisheria kati ya wakili wa serikali na wa utetezi.

Uamzi huo umefikiwa na jaji mfawidhi wa mahakama hiyo Simon Lukelewa mara baada ya kukubaliana na maombi ya wakili wa serikali Juma Masanja kwamba walichelewa kupata nakala ya maombi yaliyowasilishwa mahakama kuu na wakili wa washitakiwa.

Katika maombi yake wakili wa serikali aliiambia mahakama hiyo kuwa wao walipokea nyaraka hizo tarehe 19/07/2013  hivyo haikuwa rahisi kuweza kuzijibu na pia  aliomba wapewe nakala za mashauri mawili yaliyofunguliwa katika mahakama za wilaya ya Igunga na ile ya hakimu mkazi wa mkoa  dhidi ya wanachama hao wa Chadema.

Wakili Masanja aliiomba mahakama hiyo isiendelee kusikiliza rufaa hiyo  ya mombi ya marejeo namba 53/2013 na iwape mda ili waweze kujibu hoja zilizo wasilishwa na upande wa utetezi .

Katika maombi yao yaliyowasilishwa na wakili Peter Kibatala waliiomba mahakama kuu ipitie  majalada ya kesi hizo mbili  na hiyatolee maamuzi kwani inaonekana wameshindwa kutimiza wajibu wao.

Wakili Kibatala ameainisha katika maombi hayo kwamba kutokana na maamuzi hayo ya mahakama za chini yameathiri pia haki za waomba rufaa ikiwemo kupata dhamana.

Akitoa maamuzi ya hoja za mawakili hao aliutaka upande wa serikali uwe umejibu hoja hizo kabla ya tarehe 29/07/2013 ili ifikapo julai 30 aweze kutoa maamuzi  na kupanga tarehe ya kuanza usikilizwaji wa shauri la maombi ya marejeo lililowasilishwa na wakili Kibatala.

Watuhumiwa hao watano akiwemo kaimu katibu  wa chama hicho mkoa wa Dare salaam Henry John  Kileo wanakabiliwa na mashitaka mawili  kuwa tarehe 09-09-2011 walimjeruhi bwana Mussa Tesha  kwa kutumia tindikali na pia kutenda vitendo vya kigaidi chini ya kifungu cha nne cha sheria.

Wanachama wengine wa CHADEMA wanaokabiliwa na mashitaka hayo mawili ni pamoja na Evodius Justian, Oscar Kaijage, Seif Kabuta n Rajab Kihawa.

Akizungumza nje ya Mahakama,Wakili wa washtakiwa hao,Peter Kibatala,alisema amefurahishwa na maamuzi yaliyotolewa na jaji kwa kuonyesha kutenda haki kama ambavyo walivyotarajia kupata toka Mahakam hiyo ya juu.

Kwa upande wake Mke wa mshtakiwa Henry Kilewo, Joyce Kiria,ambaye alifika mahakamani hapo kufuatilia kesi ya mumewe aliwasisitiza wanawake wenzake kuwa wavumilivu wakati ambapo famiria zao zinapokuwa katika misuko suko ya kimaisha.

Alisema yupo naye katika kipindi hiki na bado anampenda na kuwatia moyo wanawake kuwa begakwa bega  na waume zao pale wanapokumbwa na matatizo.

Shauri hilo lilivutia umati wa wapenzi wa CHADEMA waliojitokeza kwa wingi huku ulinzi ukiwa mkali ambapo Askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia walitanda wakiwa na silaha.
 

No comments:

Post a Comment