Na Lucas Raphael.Tabora
Makala.
Januari 16 mwaka huu ni siku
ya kukumbukwa katika mkoa wa Tabora, kutokana na mkoa huo kuandika historia
mpya katika nyanja ya elimu nchini. Mkoa huo umeweza kupata Chuo kikuu cha
Kwanza toka Tanganyika ilipopata uhuru wake mwaka 1961.
Kwa muda mrefu Mkoa wa
Tabora haukuwa na vyuo vinavyotoa elimu ya juu hapa nchini hali ambayo
iliufanya mkoa huo ushindwe kupata ustawi mkubwa wa kimaendeleo ikilinganishwa
na mikoa mingine, ambayo ina vyuo vikuu.
Mkoa huo ulikuwa na vyuo
vinavyotoa elimu ya kati tu kama vyuo vya Ualimu ambavyo ni chuo cha Ualimu
Ndala, wilayani Nzega na Chuo cha Ualimu cha Tabora ambavyo vilianza kutoa
huduma hiyo kwenye miaka ya sitini na sabini.
Ukiondoa vyuo hivyo vyuo
vingine vilivyopo ni Chuo cha Utumishi wa Umma, Chuo cha Ardhi na chuo cha
kilimo Tumbi na vyuo vya ufundi vya VETA na vituo vidogo vidogo vya utoaji wa
elimu mbali mbali ndivyo vilivyokuwa vikifanyakazi ya kuwaelimisha wakazi wa
Tabora katika fani Tofauti.
Kabla ya vyuo hivyo Mkoa wa
Tabora, ulikuwa ukisifika sana kutokana na kuwa na shule mahiri za sekondari
ambazo ziliweza kuchangia maendeleo ya taifa hili kikamilifu na kwa ushindani
uliostahili.
Shule hizo ni Pamoja na
Tabora Boys, Milambo sekondari, Tabora Girls, Kazima ambazo kwa pamoja zimetoa
wataalam wengi zaidi hapa nchini pamoja na viongozi wa serikali.
Hata hivyo kukosekana kwa
elimu ya chuo kikuu katika mkoa wa Tabora, kumeufanya mkoa huo uliokuwa
ukisifika kielimu hapa nchini upoteze umaarufu wake wa miaka mingi na kujikuta
ukiwa miongoni mwa mikoa isiyokuwa tena na sifa ya kufanya vizuri katika nyanja
hiyo muhimu kwa maisha ya binadamu.
Chuo hicho kikuu
kilizinduliwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta, ambaye
ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za uzinduzi zilizofanyika
katika uwanja wa Chipukizi mjini hapa.
Katika hotuba yake waziri
Sitta, alisema kuwa hiyo ni hatua kubwa ya maendeleo katika mkoa wa Tabora,
ambao alisema umekuwa nyuma kwa muda mrefu na hivyo kuufanya usiwe miongoni mwa
mikoa yenye maendeleo makubwa kielimu hapa nchini.
Alisema kuwepo kwa chuo
hicho ni maendeleo ya kweli kwa mkoa na kuwataka wakazi wa mkoa huo kuwa makini
na kushiriki katika utoaji wa mazingira mazuri na kuwapa ushirikiano watumishi,
wahadhiri na wanafunzi ili kuongeza sifa za mkoa huo katika elimu ya juu
nchini.
Aliilaumu bodi ya mikopo
Tanzania kutokana na kushindwa kuweka mazingira mazuri ya utoaji wa mikopo kwa
wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini huku akibainisha wazi kuwa utendaji
katika bodi hiyo umejaa urasimu.
Alisema pamoja na Urasimu,
bodi hiyo imekuwa ikifanyakazi zake kwa chuki, upendeleo, dhulma na kufanya
mambo mengine ambayo hayakubaliki katika utoaji wa elimu ya juu hapa nchini.
Alisema kunahaja ya kufanya
mabadiliko makubwa katika bodi hiyo ili utendaji wake uwe na tija kwa watanzania
wanaotafuta elimu ya juu nchini ili waweze kuja kulitumikia taifa katika nyanja
mbali mbali.
Alisema suala hilo
atalifikisha serikalini kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi wa kina ambao
utasaidia kuboresha utendaji katika bodi ya mikopo nchini ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha kuwa watoto wa watanzania wananufaika zaidi na mikopo hiyo ya
kielimu.
Akizungumza katika Ibada
maalum ya ufunguzi wa chuo hicho Askofu mkuu wa kanisa Katoliki Jimbo kuu la
Tabora, Mhasham Paul Ruzoka, alisema kuwa elimu ni kitu muhimu kwa maisha ya
binadamu na kudokeza kuwa Kanisa katoliki linapenda kutoa huduma hiyo kwa
watanzania wote pasipokuwa na ubaguzi wa aina yeyote.
Alisema elimu ni kama Mwanga
unaomuwezesha mtu yeyote kuona na kufanya shughuli mbali mbali za kimaendeleo
na kijamii hapa nchini, huku akisema kuwa kinyume na elimu ni ujinga ambao
unafananishwa na giza nene ambalo linamzuia binadamu kufanya kazi mbali mbali
za maendeleo.
Askofu alisema ni wajibu wa
kila mtu kuhakikisha kuwa anapata elimu ili aweze siyo tu kuishi vizuri bali
pia kuishi maisha ambayo yatamsaidia kumjua na kumthamini Mungu ambaye ndiye
aliyejalia vipawa vya kila namna kwa binadamu.
Alisema kwa kuwa Kanisa
katoliki linatambua umuhimu wa jambo hilo litaendelea kutumia fursa zilizopo
ili kuweza kuendelea kuwasaidia wananchi waweze kupata fursa hiyo muhimu kwa
maendeleo ya umma na kuondoa ubabaishaji katika utoaji wa huduma za kijamii
miongoni mwa watanzania.
Askofu mkuu aliwahimiza
waumini wa kanisa hilo na wale ambao si waumini kukitumia vizuri chuo hicho
kikuu kwa ajili ya manufaa ya kijamii na kudokeza kuwa lengo la kanisa ni
kuhakikisha kwamba ustawi wa watu unakuwabora zaidi kadri miaka inavyoongezeka.
Akizungumza mara baada ya
ibada hiyo maalum ya kufungua chuo kikuu cha Archbishop Mihayo university
College of Tabora ( AMUCTA) ambacho kitakuwa chuo kikuu kishiriki cha mtakatifu
Augustine cha Jijini Mwanza (SAUT) Makamo mkuu wa chuo hicho nchini Dk. Charles
Kitima, alisema ni muhimu watoto wa Tanzania wakinufaika na elimu ya juu.
Alisema katika siku za
karibuni kumeibuka mtindo wa viongozi wa kiserikali kuweka vikwazo kadha wa
kadha kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanaosoma katika vyuo binafsi wasipatiwe
mikopo na kwamba wanafunzi watakaopewa mikopo ni wale wanaosoma katika vyuo na
taasisi za serikali pekee.
Alisema kauli hiyo ilipingwa
vikali na wakuu wa vyuo binafsi kwa sababu si haki kufanya hivyo na kwamba vyuo
vya elimu ya juu vya binafsi vimeanzishwa kwa ajili ya kuisaidia serikali iweze
kupata wataalam wengi zaidi.
Kulingana na Dk. Kitima,
serikali haiwezi kuwasomesha wanafunzi wote waliomaliza elimu ya kidato cha
sita na kufaulu mtihani kwahiyo ni vyema ikashirikiana na vyuo vikuu vya
binafsi vinavyowapatia vijana elimu hiyo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Alisema ni vyema basi
serikali ikajitahidi kuondoa kero hizo ndogo ndogo zinazowakabili wanafunzi
hasa katika sekta ya mikopo kwani alisema bodi ya mikopo nchini imekuwa
ikionekana kama kikwazo kwa watoto wa wakulima kupata elimu ya juu nchini
Tanzania.
Alisema mikopo ni haki yao
na kwamba wananchi wanapaswa kujua na kutambua kuwa suala la utoaji wa elimu ya
juu nchini ni la lazima na ni haki yao ya kimsingi watoto wao kuipata elimu
hiyo muhimu kwa ustawi wa taifa hili.
Alisema jamii ya wasomi
itaendelea kupinga sera mbovu ambazo hazina tija kwa taifa letu na kubainisha
kuwa jamii hiyo itaendelea kufanya utafiti utakaosaidia kuimarika kwa elimu
nchini ikiwa ni njia pekee ya kupambana na tatizo la kuwa na wataalam wasiokuwa
na sifa zinazotakiwa.
Mkuu wa chuo kikuu cha
Askofu Mkuu Mihayo cha Tabora ( AMUCTA) Dk. Thadeus Mkamwa, alisema kuwa chuo
hicho kikuu kimeanza rasmi novemba 3 mwaka jana, kwa kuanza na mafunzo ya
shahada ya kwanza ya Ualimu kikiwa na wanachuo 886.
Alisema kutokana na mikakati
ya chuo hicho kinatarajia kuanzisha pia shahada za masomo ya sayansi ya jamii,
biashara na sheria ambayo yanatarajia kuleta mapinduzi mazito katika suala zima
litakalosaidia maendeleo ya Taifa hili.
Alisema pamoja na kuanza
fani hizo, alisema katika mipango ya muda mfupi chuo hicho kitaanza kutoa
mafunzo ya elimu ya juu katika fani hizo kwa watu wa makundi maalum ambao ni
walemavu kama wasiosikia, wasiosema na wenye matatizo tofauti.
Alisema kwa mujibu muongozo
wa chuo hicho, kinapaswa kuwa na wanachuo wasiopungua 5000 kitakapokamilika
kimejikita zaidi katika ufundishaji wa masomo ya juu kwa kiwango kizuri na bila
ya kusahau suala zima la maadili ya umma.
Alisema kampasi ya chuo
hicho inatarajia kujengwa katika eneo la Kazima, umbali kama wa kilomita nane
kutoka mjini Tabora, ambapo kazi ya kulipa fidia kwa wananchi waliokuwa
wakimiliki eneo hilo ikiwa inaendelea.
Aliwataka wakazi wa Tabora
kuwatambua na kuwathamini wanafunzi wa chuo hicho, hasa pale wanapotafuta
makazi kwa ajili ya kusoma wasiwapandishie bei kwa kudhani kwamba wanapesa za
kutosha hivyo kuwakwamisha kufikia malengo yao ya kielimu.
Alisema hao ni watoto wa
masikini kama wao hivyo wanachopaswa kukifanya ni kuwasaidia na si kuwakomoa
kwani kama tujuavyo kuwepo kwa wanachuo kutasaidia pia kukuza maendeleo katika
mji huo kwa sababu mzunguuko wa pesa utaongezeka katika mji huo.
Mkuu wa Chuo, aliwataka
wanachuo kusoma kwa bidii kubwa na kuhakikisha kuwa wanapata taaluma bora zaidi
itakayowasaidia kupata uelewa mkubwa utakaosaidia kuwapa ushindani na kumudu
kufanyakazi mahali popote katika ulimwengu bila ya kuathiri mila na desturi za
wenyeji wao.
Sherehe hizo za ufunguzi wa
chuo hicho zimehudhuriwa na maelfu ya wakazi wa mji wa Tabora, viongozi wa
chama Tawala na serikali, wabunge, maaskofu wa majimbo mbali mbali nchini na
mapadri wanaoziwakilisha jumuiya mbali mbali katika jimbo Kuu la Tabora.
Mwisho.
|
Thursday, November 29, 2012
WEKEZENI ELIMU KWA WATOTO WENU MWASSA
Na Lucas Raphael ,Tabora
wekezini kwenye elimu ya watoto
Wazazi na walezi mkoani Tabora wametakiwa kuwekeza
kwenye elimu ya watoto wao kwa kufanya hivyo watakuwa wamewapata urithi wa
pekee watoto wao ,urithi huo ni mzuri kuliko mali .
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Tabora
Fatuma Mwassa wakati wa mahafali ya kwanza ya shule ya msingi ya Istiqaama
inayomilikiwa na taasisi ya kiislamu ya Istiqaama yaliyofanyika katika viwanja
vya shule hiyo jana .
Alisema kwamba kuwekeza kwenye elimu kutawasaidia
watoto wetu kuwa na akili ya kutafuta elimu na mali hata baada ya wazazi wao
kuwa hapo duniani,kwani tumeona watu wengi wanawashia watoto mali lakini mali
hizo zinatumiwa na watu wengine na watoto wanazidi kuteseka .
Alisema kwamba familia nyingi zimekuwa zitafuta
mali bila kuwekeze kwa elimu ya watoto wao na mwisho wa siku watoto wanakosa
elimu na mali walizoziacha kwani wanadhulumiwa na wale waliwaacha kusimamia
mali hizo .
Mwassa alisema kwamba iwapo wazazi watawaachia
elimu watoto wao ni vizuri na hakuna mtu wa kudhurumu elimu hiyo zaidi ya mtoto
huyo kuitumia kwa maufaa yake na taifa kwa ujumla .
Alisema kwamba hakuna mtu ambaye hajui
umuhimu wa elimu kwa maana hiyo kila mtoto anatakiwa kupata elimu iliyobora kwa
ajili ya kukabiliana na soko la ajira.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkaow a Tabora
alifanikisha kuongoza harambee na kuichangia kiasi cha shilingi milioni
25,fedha zilizopatikana zitasaidia kukamilisha ofisi na madarasa ya wanafunzi
Katika mahafali hayo watoto 42 wa eli mu wa hawali
walipatiwa vyeti kwa ajili ya kujiunga na darasa la kwanza mwakani.
Awali shekhe wa mkoa wa Tabora Shabani Salum
aliwataka wakazi wa mkoa wa tabora kuwekeza mkoani hapa tofauti na watu
wengine ambao wanawekeza katika mkoa wanayotoka .
Alisema kwamba imekumekuwe[po kasumba ya baadhi ya
watu hasa wa mkoa huu kushindwa kuwekeza katika mkoa wao na kuwekeza katika
mikoa mingine ,aliomgeza kuwekeza huo sio tatizo bali na msisahua kwenu.
Mwisho
WAZIRI WA HABARI AFUNGUA MKUTANO WA MA-RAS JIJINI DAR
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akifungua Mkutano baina ya
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na wajumbe wa Kamati za Michezo za
Mikoa Tanzania Bara “Ma-RAS” (hawapo pichani) Jijini Dar es
Salaam.Mkutano huo unalengo la kujadili maendeleo ya Michezo nchini.
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akisalimiana na RAS wa
Njombe mara baada ya kufungua kufungua Mkutano baina ya Baraza la
Michezo la Taifa (BMT) na wajumbe wa Kamati za Michezo za Mikoa Tanzania
Bara Ma-RAS Jijini Dar es Salaam.Mkutano huo unalengo la kujadili
maendeleo ya Michezo nchini. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).WAKALA WA NISHATI YA UMEME JUA WATOA MAFUNZO
Na Lucas Raphael,Tabora.
WANANCHI
waishio Vijijini wameshauriwa kuungana majirani wawili mpaka Watatu kulingana
na umbali uliopo ili kuwa na nguvu ya pamoja ya kuweza kumudu kununua vifaa vya
kutengenezea Mfumo wa Nishati ya umeme wa Jua ili kuondokana na adha ya kuishi
gizani.
Rai
hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya katika Hotuba yake
iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Ignas Kabale wakati
wa kufunga mafunzo ya Mafundi wa Nishati ya umeme wa Jua yalifanyika katika
shule ya sekondari ya Nkumba mjini hapa.
Mkuu
huyo wa wilaya anawashauri Wananchi
majirani kuungana ili kumudu gharama za vifaa vya Nishati ya umeme wa Jua kwani
kwa kufanya hivyo kutapunguza uharibifu wa mazingira unaosababaishwa na ukataji
wa miti hovyo.
Alisema
kwamba kupatika na umeme jua utawaonzea wananchi wa vijijini tija na afya kwani
kutumia tena kuni kutapungua na afya zao zitakuwa bora na mazingira yatakuwa
mazuri .
Hata
hivyo alisema kwamba kitendo cha wakala wa nishati wa umeme jua vijijini
kufunga umeme huo katika jingo la shule ya nkumba kutasaidia wanafunzi kufanya
vizuri katika masomo yao.
Alisema
kipindi shule hizo za kutwa zinaanza mazingira yake yalikuwa ni magumu sana
lakini kwa sasa shule hizo na iwapo hostel zitajengwa katika shle huyo kusaidia
sana wanafunzi wa shule.
Wahitimu
wa Mafunzo ya ufundi wa Nishati ya umeme wa Jua kutoka vijiji mbali mbali vya
Mkoa wa Tabora walipatiwa na Wakala wa Nishati ya umeme wa Jua Vijijini kwa
lengo likiwani kuwajengea uwezo Wananchi wa kutengeneza na kueneza wenyewe
Nishati hiyo vijijini .
Aidha
alisema kwamba mafunzo hayo yamefanyika kwa Nadharia na Vitendo, ambapo
Zahanati mbili na shule moja ya Sekondari katika Manispaa ya Tabora zimewekewa
mfumo wa Nishati hiyo.
Mafunzo
hayo ya siku kumi yaliwahusisha Vijana 17 kutoka maeneo mbali mbali ya vijiji
vya Mkoa wa Tabora wakiwemo Wanafunzi wa Vyuo vya ufundi stadi (VETA) ambao
watatumika kueneza Teknojia hiyo kwa Wananchi katika Vijiji vyao.
MWISHO
WADAU WA TAKWIMU NCHINI WAKUTANA KATIKA KONGAMANO LA PILI LA MWAKA JIJINI DAR LEO
Mkurugenzi
wa Takwimu nchini, Morrice Oyuke, akisoma hotuba yake kumwakilisha
Mkurugenzi Mkuu wa TAKWIMU nchini Dkt.. Albina Chuwa, wakati wa
kongamano la pili la mwaka la wadau wa TAKWIMU nchini lililofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
kutoka Benki ya Dunia, Thomas Danielewitz, akitoa hotuba yake leo
jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa kongamano la pili la mwaka kwa
Wadau wa Takwimu nchini. Kongamano hilo la siku moja limefunguliwa na
Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Saada M. Salum (hayupo Pichani).
Baadhi
ya washiriki wa kongamano la pili la mwaka unaowashirikisha Wadau wa
Takwimu nchini wakimsikilza Naibu Waziri wa Fedha Dr. Saada M. Salum
(hayupo pichani) katika ufunguzi wa kongamano hilo leo jijini Dar es
Salaam.
Naibu
wa Wizara ya Fedha Dkt. Saada M. Salum akifungua kongamano la pili la
mwaka kwa wadau wa Takwimu nchini leo jijini Dar es Salaam., ambapo
amewasisitiza wadau kutumia takwimu zilizo sahihi. Picha na Mwanakombo
Jumaa- MAELEZO
SERIKALI YAZINDUA BARAZA LA WATAALAM WA KUREKEBISHA UPEO WA MACHO KUONA,PIA YAKABIDHI MAGARI 9 NA PIKIPIKI 107 KUSAIDIA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dkt. Hussein Mwinyi akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wataalam wa
Kurekebisha Upeo wa Macho Kuona nchini leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la wataalam
wa kurekebisha upeo wa macho kuona nchini Adam Simbeye (kulia)
akiwaeleza wajumbe malengo ya baraza hilo ya kusimamia, kudhibiti na
kuratibu utoaji wa huduma bora za macho nchini yanayofanywa na baraza
hilo kwa mujibu wa sheria ya Optometria Na.12 ya mwaka 2007. Kushoto ni
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi.
Wajumbe wa Baraza la Wataalam wa
Kurekebisha Upeo wa Macho Kuona nchini wakiwa katika picha ya pamoja na
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi (Katikati) mara
baada ya kuzinduliwa kwa baraza hilo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii
Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) na mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini
Tanzania Bi.Mariam Khan (kulia) kwa pamoja wakisaini nyaraka za
kukabidhi magari 9 ya kubebea wagonjwa na pikipiki 107 kwa ajili ya
kupelekwa katika maeneo mbalimbali kusaidia huduma za afya.
Mwakilishi wa Shirika la UNFPA
nchini Tanzania Bi.Mariam Khan (kulia) akimkabidhi funguo za gari la
kubebea wagonjwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi
leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) akimkabidhi funguo za gari la kubebea
wagonjwa mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Bukombe Dkt.Archard
Rwezahura (katikati) leo jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia
makabidhiano hayo ni mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Tanzania
Bi.Mariam Khan.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
UZINDUZI WA TUSKER LITE NDANI YA USIKU WA MAAFISA MASOKO
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya bia
ya Serengeti (SBL) wakifuatilia matukio mbalimbali wakati bia mpya ya Tusker
Lite ilipozinduliwa sanjari na usiku maalum wa maafisa masoko jijini Dar es
Salaam jana
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia
ya Serengeti (SBL), Epraim Mafuru (mwenye suti kushoto) akimkabidhi zawadi ya
Tusker Lite, Meneja bidhaa wa Push Mobile, Gonzoga Rugambwa baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa shindano
maalum la uchezaji mziki lililofabnyika wakati wa uzinduzi wa bia ya Tusker
Lite sanjari na usiku wa maafisa masoko jijini Dar es Salaam jana.Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Steve Gannon akinyanyua juu bia mpya ya Tusker Lite wakati wa uzinduzi wake rasmi uliofanyika mbele ya maafisa masoko wa makampuni mbalimbali nchini wakati wa tafrija maalum ya ‘Markerts Night’ jijini Dar es Salaam jana
Vijana wa sarakasi wakionesha ufundi wao wakati wa tafrija ya maalum ya Maafisa masoko na uzinduzi wa bia mpya ya Tusker Lite inayozalisha na kusambazwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.
Wednesday, November 28, 2012
MAELFU YA WATU WAMZIKA MSANII SHARO MILIONEA KIJIJI KWAO MKOANI TANGA
Nape akimpa pole Zaina Mkieli Mama wa Hussein Ramadhani, Sharo Milionea, Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga
Baadhi ya wasanii msibani, Lusanga
DC Muheza, Subra Mgalu akisoma salam za EOTF ya Mama Mkapa
Baadhi ya wasanii msibani, Lusanga
Nape (Watatu kulia, waliobeba jeneza) akishiriki kubeba jeneza lilipofika Lusanga, nyumbani kwa marehemu
Nape akitoa pole za Chama kwenye mazishi hayo
Nape akitupa udogo kaburini wakati wa mazishi ya Sharo Milionea, Lusanga, Tanga
Waombolezaji wakaimsaidia mwenzao aliyepoteza fahamu msibani
Mwili wa SharoMilionea ukiswaliwa
Mzee Kingi Majuto akitupa mchanga kaburinu kumzika Sharo Milionea
Nape, Rais wa Bongo Movies Simon
Mwakifwamba, Meneja mahusiano wa kamuni ya Airtel,Jackosom Mbando
wakisubiri mwili wa marehemu kuwasili nyumbani Lusango, Muheza.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya
a.k.a Bongofleva Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA akitoa salam kwa niaba ya
Wanamuziki wa Bongofleva.
Kutokana na Umati wa Watu kuwa
mkubwa wengine ilibidi wapande juu ya minazi ili kushuhudia safari ya
mwisho ya Ndugu yetu Sharomilionea.Picha kwa Hisani ya jiachie Blog
EVANS BUKUKU COMMENDY CLUB YAWASHIKA WAKAZI WAPENZI WAKE NDANI YA NYUMBANI LOUNGE, DAR
Mshereheshaji Taji Liundi
akiongoza jahazi ndani Commedy live ambayo hufanyika kila mwishoni mwa
mwenzi ndani Nyumbani Lounge jijini Dar.
...Kila mmoja yupo busy akifuatilia onyesho.
Mchekeshaji wa kundi la VUVUZELA
ENTERTAINMENT linalosimamiwa na Evans Bukuku, Raymond akionyesha makeke
yake, katika onyesho lao ambalo hufanyika kila mwishoni mwa mwenzi ndani
Nyumbani Lounge jijini Dar.
...Watu waliojitokeza wakijiachia kwa kicheko.
Mchekeshaji machachali wa kundi la Vuvuzela, DOGO PEPE akiwavunja mbavu wageni waliojitokeza katika onyesho lao.
Vicheko kila mahali maana DOGO PEPE alikuja kivingine ka kuwaacha watu hoi.
Mwanadada Enika nae alitoa burudani.
Watu waliojitokeza katika onyesho hilo.
Mchekeshaji mwalikwa kutoka nchini
Kenya, Mdomo Bag akitoa burudani katika onyesho la Vuvuzela
Entertainment ambalo hufanyika kila mwishoni mwa mwenzi ndani Nyumbani
Lounge jijini Dar.
Missie Popular nae akikuwepo kutoka sapoti.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA RAIS WA KENYA MWAI KIBAKI BAADA YA UFUNGUZI WA OFISI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI, JIJINI ARUSHA JANA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Rais wa Kenya, Mwai Kibaki, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro, mara baada ya ufunguzi wa Jengo la ofisi za Jumuiya hiyo
iliyofanyika Jijini Arusha jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimsindikiza Rais wa Kenya, Mwai Kibaki, ambaye ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro, mara baada ya ufunguzi wa Jengo la ofisi za Jumuiya hiyo
iliyofanyika Jijini Arusha jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipunga mkono kuwaaga wananchi baada ya kumsindikiza Rais wa Kenya,
Mwai Kibaki, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, mara baada ya
ufunguzi wa Jengo la ofisi za Jumuiya hiyo iliyofanyika Jijini Arusha
jana.
Subscribe to:
Posts (Atom)