Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Gharib Bilal na Mkewe
mama Aisha Bilal wakishuka kwebye ndege mara baada ya kuwasili kwenye
uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi kwa ajili ya uzinduzi wa mkoa
mpya wa Katavi unaofanyika mjini mpanda kesho, Makamu wa Rais pia
amezinddua uwanja wa ndege wa Mpanda na kuzindua Kongamano la Tathimini
ya Mkutano wa Uwekezaji Ukanda wa Ziwa Tanganyika uliofanyika Oktoba 17
mwaka jana na kushirikisha mikoa mitatu ya Rukwa, Kigoma a kufanyika
mjini mpanda ambapo sasyamekuwa makao makuu ya Mkoa wa Katavi
Makamu
wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda
mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda, kushoto ni Mkuu
wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe na katikati ni mama Tunu Pinda.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal
kushoto akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa
Kongamano la kutathmini Mafanikio na Changamoto baada ya mkutano wa
Uwekezaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika Kigoma na Rukwa uliofanyika
Oktoba 17 mwaka jana mjini Mpanda
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akizungumza katika uzinduzi wa Uwanja wa ndege wa
Mpanda, kshoto ni Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal na kulia ni mama
Zakia Bilal.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza wakati wa uzinduzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi leo mchana.
Katibu
Mkuu Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar Chambo akitoa taarifa ya ujenzi
wa uwanja huo kwa Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal wakati wa uzinduzi
mjini mpanda leo.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba akimkaribisha Makamu wa Rais ili
kuongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa uwanja huo mjini Mpanda leo
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi
wa uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kukamilika kwa ujenzi wa uwanja
huo, kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo
Pinda na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba, kushoto ni Mama
Zakia Bilal mke wa Makamu wa Rais.
Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye, Dkt. Mary
Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Mama Tunu
Pinda Mke wa Waziri Mkuu na Mama Zakia Gharib Bilal Mke wa Makamu wa
Rais wakiwa katika uzinduzi huoMakamu
wa Rais akisalimiana na Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwekezaji mara
baada ya kuwasili mjini Mpanda leo Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Katavi
Mselem na kutoka kulia ni Mbunge wa Mpanda mjini CHADEMA Mh.Said Arfi
na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt Charles Tizeba.
Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal akivishwa skafu na vijana wa chipukizi mjini Mpanda mara baada ya kuwasili mkoani Katavi leo.
Makamu
wa Rais akisalimiana akipungia mkono wananchi waliofika kumlaki kwenye
uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi leo, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa
Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa Bw. Mselem.
Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal na Mkewe Mama Zakia Bilal wakiangalia ngoma katika uwanja wa ndege wa Mpanda
Mama
Tunu Pinda akishiki kuchza ngoma za asili za mkoa wa Katavi kwenye
uwanja wa ndege wa Mpanda wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais Dkt.
Gharib Bilal.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Kyando Mchechu
Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akifurahia jambo na Mzee Paul Kimiti Waziri Mkuu
wa Zamani na Mbunge wa jimbo la Sumbawanga miaka iliyopita kwenye
uwanja wa ndege wa Mapanda
Makamu
wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mh.
Venance Mwamoto wakati wa mapokezi hayo, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Dkt Rajab Rutengwe.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akimpa ishara ya Dole Mbunge wa Mpanda mjini CHADEMA
Mh. Said Arfi, wakati wa mazungumzo yao kwenye uwanja wa ndege wa
Mpanda katika mapokezi ya Makamu Wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Kauli mbiu
ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutegwe katika maendeleo mkoani
Katavi inasema "SIASA NI MAENDELEO"
kutoka
kulia ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injini Stella Manyanya, Mkuu wa mkoa wa
Katavi Dkt. Rajab Rutengwe, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya
na mwenyekiti wa CCM Mpanda Hamida Mbogo wakizungumza mawili matatu
wakati wa mapokezi ya makamu wa Rais mjini Mpanda leo,
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Mzee Chrisant Mzindakaya ambaye ni
mwekezaji mkoani Rukwa na wwekezaji wengine kutoka India, kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe akizungumza katika kongamano hilo
kwenye ukumbi wa Idara ya maji mjini Mpanda na kukaribisha wageni
mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo.
Mkuu
wa mkoa wa Rukwa Injini Stella Manyanya akizungumza na kutoa taarifa ya
mkoa wake katika suala zima la uwekezaji mkoani Kwake
Waziri
wa Uwezeshaji na Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Mary Nagu
akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika mjini Mpanda leo
Mabalozi
mbalimbali wamehudhuria katika sherehe hizo za uzinduzi wa mkoa wa
Katavi kutoka Burundi, Zambia, Misri, Japan na DRC Kongo
No comments:
Post a Comment