Brass Band ya Jeshi la Polisi
ikiongoza maandanamo ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake
yaliyoratibiwa na Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya
Afrika (WILDAF),yaliyoanzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na
kumalizikia kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
Maandanamo yakipokelewa na
Muwakilishi wa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Mambo ya Ulaya na
Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Dora
Msechu (wa tatu kulia),Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria
na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula,Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema (pili kulia) pamoja na
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Charles Kenyera.
Balozi wa Ireland nchini,Mh.
Fionnuala Gilsenan akikata utepe uliokuwepo kwenye basi aina ya Toyota
Coster,ikiwa ni uzinduzi rasmi wa Safari ya Wadau wa Wildaf wanaokwenda
Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya Kuendelea kutoa Mafunzo kwa
Watu mbali mbali katika mikoa ya kanda hiyo kuhusiana Ukatili dhidi ya
Wanawake.
Mgeni
rasmi katika Mkutano huo,ambaye ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh.
Angella Kairuki akisoma Hotaba yake mbele ya Mamia ya Wadau wa Wildaf
waliohudhulia Mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini
Dar es Salaam.Wengine Pichani toka kulia ni,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema,Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula na Mkurugenzi wa Mambo ya Ulaya na Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Dora Msechu.
Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake
Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula
akisisitiza jambo wakati akitoa neno la Ukaribisho katika Mkutano wa
Wadau wa Wildaf wenye kauli mbiu isemayo "FUNGUKA - Kemea Ukatili Dhidi
ya Wanawake !!,Sote Tuwajibike" uliofanyika mapema leo,kwenye Ukumbi wa
Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuliwa na Wadau mbali
mbali.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la
Polisi nchini,DCP Rashid Omar akiwasilisha mada ya aina mpya ya Karatasi
maalum itolewayo na Polisi iwapo mtu anapatwa na tatizo la Majeraha (PF
3) iliyofanyiwa Marekebisho na kuongezewa baadhi ya Vipengele
Muhimu,wakati wa Mkutano uliofanyika leo wa Kupiga Vita Ukatili dhidi ya
Wanawake,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment