Mke wa balozi wa Ireland nchini
Tanzania (wa kwanza kushoto), Sarah Colins akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari, uliofanyika katika ubalozi wa Uswisi, kuhusu
maonesho ya hisani yatakayonyika siku ya jumamosi jijini Dar es Salaam
yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watu wanaoishi katika
mazingira magumu .na kufunguliwa na mke wa Makamu wa Rais Bi. Asha Bilal
siku ya jumamosi. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa kundi hilo Juliana
Parroni (Switzeland) na Keiko Okada (Japan).
Mwenyekiti wa kundi la wake wa
mabalozi nchini (DSG) Juliana Parroni,(kulia) akizungumza na waandishi
wa habari, juu ya maonyesho ya hisani yatakayo fanyika siku ya jumamosi
na kufunguliwa na Mke wa makamu wa Rais, Bi Asha Bilal kwa ajili ya
kuchangisha fedha kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu. Kutoka
kushoto ni mke wa Balozi wa Namibia Aletha Aisaack, Sara Colins
(Ireland) Keiko Okada (JAPAN) na Kaisa Alapartanen (Finland).
Mke wa Balozi wa Japani nchini
Tanzania (wa kwanza kutoka kulia) Keiko Okada, akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari juu ya Maonyesho ya hisani
yatakayofanyika mwisho wa wiki ili kuchangisha fedha kwa ajili ya
makundi ya watu wasiojiweza, pamoja nae kutoka kushoto ni Mke wa Balozi
waIreland Sarah Colins na katikati ni Mwenyekiti wa umoja huo Bi.
Juliana Paroni. Maonyesho hayo yatafunguliwa na Bi. Asha Bilal Mke wa
makamu wa Rais.
======== ======= =======
Maonyesho ya Hisani 2012
Siku ya furaha kwa mafanikio ya Watanzania.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania, Bi. Asha Bilal, anatarajia kuwa Mgeni rasmi
katika Maonyesho ya Hisani yaliyoandaliwa na kundi la wake wa
Mabalozi nchini. (DSG)
Maonyesho hayo yatakayo fanyika
Novemba 17, mwaka huu katika viwanja vya Shule ya Kimataifa ya
Tanganyika, jijini Dar es Salaam, hufanyika kila Mwaka kwa ajili ya
kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jamii zenye mahitaji maalumu
hasa wanawake, watoto na walemavu wanaoishi katika mazingira magumu
ikiwa ni mala ya pili Mke wa Makamu wa Rais kuendesha uchangishaji huo.
Mwaka 2011, Umoja huo kupitia
maonyesho ya hisani ulikusanya jumla ya Shilingi milioni 73, ambazo
zilisambazwa kama ufadhili kwenye miradi 15 ya hisani na taasisi binafsi
Tanzania Bara na Visiwani, michango hiyo hufikia shilingi milioni 15
kwa kila kundi.
No comments:
Post a Comment