Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo
Mmoja wa maofisa wa TGNP kutoka Idara ya Habari na Mawasiliano, Deo
Temba (kushoto) akichukua kumbukumbu katika mkutano huo na wahariri.
Pembeni yake ni Prof. Ruth Meena
Mmoja wa wahariri kutoka vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Jane Mihanji na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa
Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) akichangia mada katika
mkutano
Mwandishi wa habari na mmiliki wa Francis Godwin Blog akiwa katika mkutano huo
Prof. Meena (kulia) akifafanua jambo
Prof. Meena Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TGNP, Profesa Ruth Meena pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa TGNP, Mary Nsemwa.
Na Mwandishi wa
Thehabari.com
KAIMU Mkurugenzi
wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Mary Nsemwa amevipongeza vyombo mbalimbali
vya habari nchini kwa kile sasa kutoa nafasi ya kuridhisha kwa kuandika masuala
mbalimbali ya kijinsia ambayo hapo awali yalikuwa hayapewi nafasi ya kutosha.
Bi. Nsemwa
ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wahariri
mbalimbali wa vyombo vya habari katika mkutano wao na TGNP, kuzungumzia
changamoto anuai za kijinsia na vyombo vya habari pamoja na ushiriki wa
wanawake katika mchakato wa maoni ya uundwaji wa katiba mpya.
Alisema
ushirikiano mzuri uliojengeka kati ya taasisi hiyo na vyombo vya habari
umesaidia kwa kiasi kikubwa hivyo masuala ya kijinsia na hasa yale
yanaowakandamiza wanawake kusikika katika vyombo vya habari hali ambayo
imesaidia kwa kiasi fulani.
“…Tumejifunza
mengi kutoka katika vyombo vya habari, vyombo hivi sasa vimewaunganisha
wanawake…sauti za wasiosikisa hasa wa vijijini sasa zinasikika kupitia vyombo
hivi. Vyombo vya habari pia vimepaza sauti kwa kampeni yetu ya Haki ya Uchumi; ‘Rasilimali
Ziwanufaishe Wanawake walioko Pembezoni’ na mkumbuke kwamba nyinyi mnanguvu
zaidi yetu,” alisema Bi. Nsemwa.
Naye mmoja wa
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Profesa
Ruth Meena akiwasilisha mada katika mkutano huo wa wahariri alisema mambo mengi
ya msingi ambayo ni miongoni mwa madai ya wananchi yameainishwa katika Katiba
iliyopo sasa, hivyo kushauri ipo haja ya kuangalia namna ya usimamizi wa sheria
na mabadiliko kadhaa kuingizwa kwenye Katiba Mpya.
“...Kwa upande mmoja Katiba Ya
Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inatoa haki sawa kwa wanawake na
wanaume katika nyanja za siasa, uchumi na ustawi wa jamii, na hapohapo kuzipokonya kwa mkono mwingine kwa kuruhusu
kuendelezwa kwa sheria, taratibu na tabia zinazokinzana na katiba,” alisema
Prof. Meena.
Aidha alishauri Katiba mpya ibatilishe sheria zote zinazokinzana na haki za
msingi za wanawake na watoto wa kike hususani kubatilisha sheria na mila zote
za ubaguzi wa jinsia, ubaguzi dhidi ya watoto hususani watoto wa kike, katika
maswala ya ndoa, mirathi, haki za kumiliki.
“Kwa mantiki hii, katiba ibainishe kwa uwazi haki za wanawake na haki za
watoto. Pamoja na kuwajibisha serikali kuchukua hatua zote za kisera na sheria
ili kulinda na kuhifadhi haki za wanawake na za watoto katika maeneo hayo, na pia iwajibishe serikali kutekeleza mikataba yote iliyoridhia kuhusu haki za
wanawake ( CEDAW, CRC, ILO Conventon) Mikataba hii itambulike kuwa ni sheria za
nchi ili kuepusha ucheleweshaji wa
kutafsri au kuruhusu uchakachuaji wamikataba hii katika sheria za nchi,”
alifafanua Prof. Meena.
Pamoja na hayo alishauri Katiba mpya iangalie haki ya
ufikiaji wa huduma za jamii; haki ya kufikia na
kufaidi huduma za msingi kama vile maji,
chakula, malazi na elimu na hifadhi ya jamii ziendelee kuwepo - pamoja na
kusisitiza wajibu wa serikali wa kuhakikisha huduma hizi za msingi
zifikiwe na ke na me ( rika zote, na
hali zote).
-Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment