Waziri
wa maliasili na Utali Mh. Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika
uzinduzi wa Mkakati wa mpya wa Utangazaji wa Kimataifa wa Utalii wa
Tanzania (International Marketing Strategy For Tanzania)mpango
uliozinduliwa jioni hii na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwenye hoteli
ya Serena jijini Dar es salaam na kujumuisha wadau mbalimbali
wanaojihusisha na masuala ya utalii ambapo Waziri Kagasheki ameuzindua
rasmi.
Waziri
wa maliasili na Utali Mh. Balozi Khamis Kagasheki akikata utepe katika
kitabu kinachoelezea mkakati wa kutangaza utalii wa utalii wa Tanzania
kimataifa kutoka kulia ni Bw. Gaudence Temu Mwenyekiti wa Shirikisho la
vyama vya Utalii Tanzania (TCT), Ahmad Khatib Kamishna wa Utalii na
kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dkt. Aloyce Nzuki.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Balozi Charles Sanga akizungumza
katika uzinduzi huo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dkt. Aloyce Nzuki akimkaribisha Waziri
wa Maliasili na Utalii ili kuzungumza na wageni waalikwa na wadau
mbalimbali katika uzinduzi huo.
Bw.
Gaudence Temu Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania
(TCT) akielezea mkakati wa kutangaza utalii wa Tanzania kimataifa kwa
wadau wa masuala ya utalii waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi
wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Ibrahim Mussa
akikaribishwa katika uzinduzi huo na Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya
Utalii Tanzania TTB Bi Devotha Mdachi
Meneja
Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw Geofrey Meena kushoto na
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Utalii Tanzania TCT Bw. Richard Rugimbana
wakifuatilia kwa karibu maelezo yaliyokuwa yakitolewa katika uzinduzi
huo.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dkt. Aloyce Nzuki akisalimiana na mjumbe
wa bodi ya wakurugenzi ya TTB . Bi. Teddy Mapunda, katikati ni Godfrey
Simbeye Mkurugenzi Asasi ya Sekta Binafsi Tanzania Private Sector
Foundation na Dan Kisirye kutoka International Finance Corporation.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki akiwa katika picha
ya pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya utalii Balozi Charles Sanga katikati
na Mjumbe wa Bodi hiyo Bi. Teddy Mapunda.
Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na Mbunge wa Mafia na Mjumbe wa Bodi ya (TTB) Mh. Abdulkarim Shah
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Utalii Tanzania TCT Bw. Richard Rugimbana kulia
akijadiliana jambo na Dan Kisirye kutoka International Finance
Corporation, katikati ni Godfrey Simbeye Mkurugenzi Asasi ya Sekta
Binafsi Tanzania Private Sector Foundation.
Kutoka kulia ni wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Karaze, Beatrice na Fatma wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwenyekiti
wa bodi ya utalii Balozi Charles Sanga akizungumza jambo na Mbunge wa
Mafia na Mjumbe wa Bodi ya (TTB) Mh. Abdulkarim Shah, kulia ni
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dkt Aloyce Nzuki.
No comments:
Post a Comment