Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wageni waalikwa wakati wa
uzinduzi wa mpango kabambe wa Teknohama katika Sekta ya Elimu nchini
uliofadhiliwa na Kampuni ya HUAWEI kutoka China Katika Mradi huo wa Teknohama itayowezesha
Watanzania mbalimbali kutoka shule za Sekondari na Vyuoni kupata vifaa na
mafunzo ya Sayansi na Teknolojia ili kusukuma mbele maendeleo katika nyanja za
Uchumi na Kijamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUAWEI
kutoka China Bw. Bruce Zhang akizungumza katika hafla hiyo kwamba Mpango huu
unaoitwa "Huawei ICT Star" itasaidia katika shule za Primary na Sekondari katika
kusukuma mbele maendeleo ya Sayansi na Teknolojia nchini
Tanzania.
Alisema katika Program hii itasaidia
kuboresha miundo mbinu katika Sanyansi na Teknolojia ili kutoa mwamko kwa vijana
wa Kitanzania kujifunza masomo ya Sayansi na
Teknolojia.
Balozi wa China nchini Tanzania Mh. LU
YOUQING akitoa maelezo yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa Teknohama katika
shule na vyuo nchini Tanzania. Balozi alisema mpango huu ni mwendelezo wa
uhusiano mwema kati ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa China katika nyanja
mbalimbali za biashara uchumi na Kijamii. Aliongeza kwamba Serikali ya China
itaendelea na mikakati yake ya kusaidia nchi ya Tanzania ili kuweza kufikia
malengo ya Milenia ya 2015.
Meza kuu.
Mgeni rasmi Mh. Mbarawa na Balozi wa
China wakizindua rasmi mpango wa "HUAWEI ICT STAR" nchini
Tanzania.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia Profesa Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI Bw. Bruce Zhang
wakitiliana saini kitabu cha makubaliano rasmi ya Ushirikiano katika Sekta ya
Sayansi na Teknolojia kupitia Elimu.
Profesa Mbarawa akimkabidhi zawadi kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI.
Pichani Juu na Chini ni wageni waalikwa
waliohudhuria uzinduzi huo.
Mgeni rasmi Waziri Mbarawa akiondoka
ukumbi baada ya uzinduzi.Picha na Zainul A. Mzige.
No comments:
Post a Comment