MWANAMUZIKI nguli wa dansi
Afrika, JB Mpiana akiwa na Bendi yake ya Wenge BCBG anatarajiwa kuwasili
nchini leo kwa ajili ya maonesho matatu tofauti ikiwa ni pamoja na
litalofanyika Ijumaa kwenye Viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana
Mkurugenzi wa Kampuni ya QS J Mhonda, Joseph Mhonda alisema kuwa
mwanamuziki huyo atawasili nchini kwa kutumia ndege ya Shirikika la
Ndege la Kenya.
Mhonda alisema kuwa katika Onesho
hilo ambalo litakuwa sambamba na uzinduzi wa Albamu ya Bendi ya Mashujaa
ijulikanayo kama Risasi Kidole.
Alisema kabla ya kufanyika kwa
onesho la jijini Dar es Salaam, JB Mpiana na Bendi nzima ya Wenge BCBG
wataelekea MKoani Arusha ambako watafanya onesho maalum siku ya Alhamis
na Ijumaa kufanya mambo yake katika viwanja vya Leaders Club, Dar es
Salaam na baadaye Mwanza Desemba 2.
Mhonda alisema wakiwa MKoani
Arusha watafanya onesho hilo katika Ukumbi wa Tripple A na Mkoani Mwanza
watakuwa kwenye Ukumbi wa Villa Park.
Alisema kuwa kila kitu
kimekamilika kuhusu ujio wa mwanamuziki huyo, ambaye atakuja na
Wanamuziki wake wote 25 ambao yupo nao katika bendi hiyo.
Alisema wameona ni bora aanze
mikoani na baadae amalizie hapa na kuondoka zake katika ziara za nchi
nyingine. Mhando alisema mwanamuziki huyo atawasiri nchini na wanamuziki
wake kutoa burudani ya aina yake.
Wakati JB akiwasili leo na Bendi
ya Mashujaa chini ya Charles Gabriel ‘Chaz Baba’, wameingia kambini jana
kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi huo.
Akizungumzia kwa upande wao Chaz
baba alisema kuwa bendi hiyo ipo hapa hapa jijini Dar es Salaam, kwa
ajili ya kufanya mazoezi maalum ya uzinduzi.
Chaz Baba alisema wamejipanga kufanya uzinduzi wa aina yake katika albam yao hiyo ya pili huku kwa upande wake ikiwa ya kwanza.
"Leo (Jana) ndiyo tumeingia
kambini kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wetu kubwa ni kwamba
tumejipanga kufanya kweli katika uzinduzi huo ambao kwa upande wangu ni
wa kwanza katika bendi ya Mashujaa"alisema Chalz Baba.
Alisema albamu yao, wanayozindua
iitwayo Risasi Kidole ina nyimbo sita, ambazo ni Risasi Kidole yenyewe
utunzi wake Chaz Baba, Ungenieleza utunzi wake Raja Ladha, Umeninyima
utunzi wa Freddy Masimango, Hukumu ya Mnafiki utunzi wake Jado FFU, Kwa
Mkweo utunzi wake Baba Isaya na Penzi la Mvutano, ambao umetungwa na
Masoud Namba ya Mwisho.
Chaz Baba alisema kama
ilivyopangwa, mbali na JB Mpiana, wanamuziki wengine watakaopamba
uzinduzi huo ni MB Dogg, H Baba, Ney wa Mitego na wengineo ambao
watajulikana baadaye.
“Sisi kwa upande wetu tumejipanga
vizuri kuwapa watu burudani ambayo tunajua kwa muda mrefu wameikosa,
Mashujaa tunakuja kushujaa, ushujaa wa kuwaburudisha watu na kukata
kabisa kiu yao,”alisema Chaz Baba.
Alisema wanataka kufanya shoo
ambayo hata JB mwenyewe akiona atakubali kwamba Tanzania kuna bendi
yenye ubora sawa na bendi za kwao, Kongo, ambayo ni Mashujaa.“Hadi sasa
wapenzi wa muziki hapa Dar es Salaam ambao wamebahatika kuona shoo zetu
wanakiri sisi ndio mabingwa wapya wa muziki wa dansi Tanzania, sasa
tunataka tumdhihirishie hilo na JB Mpiana,”alisema Chaz Baba.
No comments:
Post a Comment