Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M.
Haule, akifungua Mkutano wa Timu ya Pamoja ya Wataalam kati ya
Tanzania na Malawi kuhusu mgogoro wa mpaka kwenye Ziwa Nyasa. Mkutano huo uliowahusisha wataalam kutoka Wizara na
Idara mbalimbali za Serikali za Tanzania na Malawi unafanyika
Jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena.
Bw. Julius Chisi, Naibu Mpimaji Ardhi Mkuu kutoka Malawi akizungumza machache wakati wa mkutano huo.
Bw. Abdallah Mtibora, Afisa kutoka
Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa
akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa kufungua mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania
akiwemo Mhe. Balozi Patrick Tsere (wa pili kutoka kushoto), Balozi wa
Tanzania nchini Malawi na Balozi Irene Kasyanju (kushoto) wakimsikiliza
Bw. Chisi (hayupo pichani) wakati wa akizungumza.
Baadhi ya Wajumbe wengine kutoka Malawi akiwemo Mhe. Chiyaonga (kulia), Balozi wa Malawi hapa nchini.
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe kutoka Malawi wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule akizungumza na Mhe.
Flosie Gomile Chiyaonga, Balozi wa Malawi hapa nchini kabla ya kuanza
kwa Mkutano wa Timu ya Pamoja ya Wataalam wa Tanzania na Malawi kuhusu
mgogoro wa mpaka kwenye Ziwa Nyasa.Picha na Habari- Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
--
Mkutano kati ya Tanzania na Malawi kujadili suluhu ya mgogoro
wa mpaka kwenye Ziwa Nyasa umeanza katika ngazi ya Wataalamu jijini Dar es
Salaam tarehe 15 Novemba, 2012.
Mkutano huo unaowahusisha
wataalam kutoka Wizara na Idara mbalimbali za Serikali za Tanzania na Malawi unafanyika Jijini Dar
es Salaam katika Hoteli ya Serena.
Akifungua Mkutano huo Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule alisisitiza
umuhimu wa wajumbe kutoka nchi zote mbili kujadili na kupendekeza njia
zitakazosaidia kupata suluhisho la kudumu la mgogoro huo.
Aidha, Bw. Haule aliweka bayana kuwa
Serikali ya Tanzania ina
dhamira ya dhati kufanya kazi pamoja na Serikali ya Malawi kutafuta suluhu ya mgogoro
huo jambo ambalo pia lilisisitizwa na Bw. Julius Chisi, Kiongozi wa Ujumbe wa
Malawi.
Mkutano huo ambao utafanyika kwa siku tatu
hadi tarehe 17 Novemba, 2012 umeanza na Kikao cha Wataalamu ambacho kitafuatiwa
na kikao cha Maafisa Waandamizi na kuhitimishwa na kikao cha Mawaziri tarehe 17
Novemba, 2012.
No comments:
Post a Comment