Wafanyabiashara
wawili wa Jijini Dar es Salaam, wametiwa mbaroni Visiwani Zanzibar
baada ya kupatikana wakiingiza madawa ya kulevya kwa njia ya majini.
Naibu
Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Zanzibar ACP Yusuf Ilembo, amewataja
watuhumiwa hao kuwa ni Othuman Chande Othmani (22) mkazi wa Kinondoni na
Abubakari Muharami Bakari(33) mkazi wa Temeke.
Kamanda
Ilembo amesem,a kuwa watuhumiwa hao wote wamekamatwa katika Bandari ya
Zanzibar walipokuwa wakiwasili kwa boti kutoka Dar es Salaam wakiwa na
madawa hayo ya kulevya aina ya Heroine.
Amesema
kuwa Mtuhumiwa Abubakari alikamatwa juzi saa 3.00 asubuhi akiwa na
kifurushi kimoja likichokuwa na madawa hayo ambapo mwenzake Othman yeye
ametiwa nguvuni leo saa 3.00 asubuhi akiwa na vifurushi viwili vya
madawa hayo aina ya Heroine.
Kamanda
Ilembo amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na kuimarishwa
kwa ulinzi na upekuzi wa hali ya juu uliopo katika maeneo ya viwanja vya
ndege na bandari ya Zanzibar.
Amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao za kupatikana na madawa ya kulevywa visiwani hapa.
Amewataka
wananchi wakiwemo wasafiri wa ndege na boti wanaoingia na kutoka katika
visiwa vya Unguja na Pemba kuacha kulalama na kuona kuwa wanapopekuliwa
wanabughudhiwa.
Ammesema
maeneo yote ya Viwanja vya Ndege na Bandarini Jeshi la Polisi kwa
kushirikiana na Maafisa wengine wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama
vimeimarisha ulinzi ili kuhakikisha kuwa hakuna kitu cha hatari
kinachoingizwa Visiwani humo.
Mbali
ya Madawa ya kulevya na silaha, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imepiga mariufuku uingizwaji wa mifuko ya plastiki ya aina zote na
kwamba kwa yeyote atakayepatikana na mfuko wa plastiki atakamatwa na
kufikishwa mahakamani.
Kwa
siku za hivi karibuni baadhi ya wasafiri wamekuwa wakilalamikia hali ya
upekuzi unaoendeshwa katika maeneo ya Viwanja vya Ndege na Bandari na
hali wanayoona kuwa ni usumbufu kwao.
KWA UFAFANUZI ZAIDI, WASILIANA NAMI KWA SIMU ZIFUATAZO
0715 886488, 0784 886488, 0767 886488, 0774 886488 INSP. MHINA
No comments:
Post a Comment