Thursday, November 29, 2012

WAKALA WA NISHATI YA UMEME JUA WATOA MAFUNZO

Na Lucas Raphael,Tabora.

WANANCHI waishio Vijijini wameshauriwa kuungana majirani wawili mpaka Watatu kulingana na umbali uliopo ili kuwa na nguvu ya pamoja ya kuweza kumudu kununua vifaa vya kutengenezea Mfumo wa Nishati ya umeme wa Jua ili kuondokana na adha ya kuishi gizani.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya katika Hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Ignas Kabale wakati wa kufunga mafunzo ya Mafundi wa Nishati ya umeme wa Jua yalifanyika katika shule ya sekondari ya Nkumba mjini hapa.

Mkuu huyo wa wilaya  anawashauri Wananchi majirani kuungana ili kumudu gharama za vifaa vya Nishati ya umeme wa Jua kwani kwa kufanya hivyo kutapunguza uharibifu wa mazingira unaosababaishwa na ukataji wa miti hovyo.

Alisema kwamba kupatika na umeme jua utawaonzea wananchi wa vijijini tija na afya kwani kutumia tena kuni kutapungua na afya zao zitakuwa bora na mazingira yatakuwa mazuri .

Hata hivyo alisema kwamba kitendo cha wakala wa nishati wa umeme jua vijijini kufunga umeme huo katika jingo la shule ya nkumba kutasaidia wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.

Alisema kipindi shule hizo za kutwa zinaanza mazingira yake yalikuwa ni magumu sana lakini kwa sasa shule hizo na iwapo hostel zitajengwa katika shle huyo kusaidia sana wanafunzi wa shule.

Wahitimu wa Mafunzo ya ufundi wa Nishati ya umeme wa Jua kutoka vijiji mbali mbali vya Mkoa wa Tabora walipatiwa na Wakala wa Nishati ya umeme wa Jua Vijijini kwa lengo likiwani kuwajengea uwezo Wananchi wa kutengeneza na kueneza wenyewe Nishati hiyo vijijini .

Aidha alisema kwamba mafunzo hayo yamefanyika kwa Nadharia na Vitendo, ambapo Zahanati mbili na shule moja ya Sekondari katika Manispaa ya Tabora zimewekewa mfumo wa Nishati hiyo.

Mafunzo hayo ya siku kumi yaliwahusisha Vijana 17 kutoka maeneo mbali mbali ya vijiji vya Mkoa wa Tabora wakiwemo  Wanafunzi wa Vyuo vya ufundi stadi (VETA) ambao watatumika kueneza Teknojia hiyo kwa Wananchi katika Vijiji vyao.

 MWISHO

No comments:

Post a Comment