Sina shaka ndugu zangu mtakubaliana nami endapo kama nawakilisha wazo langu juu ya uhatari wa watoto unaowazunguuka kwasasa ambapo kwa namna moja ama nyingine inaonekana kuwa ni jambo la kawaida katika maisha ya kila siku kawenye jamii zetu.
Tunaweza kuwa tunalaumu kuwa watoto hawapati elimu ya kutosha kumbe baadhi ya mambo huenda tukawa tunayasababisha sisi wenyewe....kwa mfano:-Baadhi ya watu wanadai kuwapa ajira watoto eti kwa kigezo cha kuwasaidia,hili jambo binafsi siliafiki kabisa.
Najaribu kuliweka sawa hili,eti mtoto inakuaje anapata pesa za kununua sigara dazeni kadhaa na kuziweka kwenye ungo na kutambua kuwa kila siku auze kiasi gani,apange kiasi kipi cha kuendeleza mtaji huo kama sio sisi wenyewe watu wazima kuwapatia ajira hiyo ya kutembea sigara takribani zaidi ya saa 14 kila siku na tena kwenye baadhi ya mabanda ya kuuzia vinywaji vya ulevi.
Pengine hatuoni kuwa ni hatari wakati mtoto huyu anayefanya biashara ya aina hii na nyinginezo kuwa huenda akajifunza tabia hatarishi huko anakopitapita.
Achana na hilo ebu jaribu kuangalia hili tena....Eti mzazi anadiriki kumtuma mtoto wake bia au ulevi wa aina yeyote grocery,na tena baada ya kuleta anaagizwa afungue hicho kinywaji na kukimimina kwenye glasi.
Kwanini mzazi asiende huko bar au grocery akafanye anavyotaka na sio kumgeuza mtoto kuwa bamedi wa ndani ya bar isiyo sajiriwa,....hatulioni hili kuwa ni tatizo
Hivi ni wakati gani watu wataona kuwa njia nzuri ya kumsaidi mtoto ni hii au ile..........au hivi sheria zilizotungwa kwa ajili ya kuwalinda watoto hazitekelezwi au zinatekelezwa kwa namna gani,au ndio kusema hata mzazi akifanya chochote kwa mtoto wake ni sawa kwakuwa amemzaa mwenyewe,hapana tujaribu kuangalia kwanza wakati huu tunaandaa kizazi kitakachokuwa kwenye dimbwi baya kwa kuwafanyia ukatili hawa watoto wetu.
No comments:
Post a Comment