Monday, November 26, 2012

RC FATMA MWASSA ACHANGISHA ZAIDI YA MIL.25 UJENZI WA SHULE YA KIISLAM ISTIQAMA TABORA


 Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Abubakari Mwassa akimpatia cheti cha kuhitimu elimu ya awali Fatma Abubakari katika mahafali Shule msingi ya Istiqama Muslim ya mjini Tabora.
 Wahitimu wa elimu ya awali  Shule ya msingi Istiqama Islamic wakiwa katika mahafali baada ya kupokea vyeti vya kuhitimu na kujiunga na elimu ya darasa la kwanza.
 Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa akiongoza  harambee wakati wa mahafali hayo ambapo zilichangwa zaidi ya shilingi mil.25 kwa ajili ya ujenzi wa Shule hiyo inayomilikiwa na waislamu nchini.
 Baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu mkoani Tabora wakiwa na viongozi wa serikali katika mahafali hayo.
 Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Bw.John Mchele akitoa tamko la kuchangia katika harambee hiyo.

 Mwenyekiti wa bodi ya Shule ya Istiqama Sheikh Mohammed Mbega akitoa taarifa fupi ya shule hiyo tangu kuanzishwa kwake.
 Mjumbe wa bodi ya shule ya Istiqama Islamic ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni la usafirishaji la NBS Tabora Bw.Nassor Hamdan akitoa zawadi kwa baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Katikati ni mmoja wa viongozi wa Shule ya msingi Istiqama Bw.Humud Super Sonic,kushoto ni Mkurugenzi wa Tabora Tv Bw.Shashikant Patel na kulia ni mtangazaji wa Radio V.O.T Bw.Vituko Salala. 

Na Lucas Raphael,Tabora




Wazazi na walezi mkoani Tabora wametakiwa kuwekeza kwenye elimu ya watoto wao kwa kufanya hivyo watakuwa wamewapata urithi wa pekee watoto wao ,urithi huo ni mzuri kuliko mali .

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Tabora Fatuma Mwassa wakati wa mahafali ya kwanza ya shule ya msingi ya Istiqaama inayomilikiwa na taasisi ya kiislamu ya Istiqaama yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo jana .

Alisema kwamba kuwekeza kwenye elimu kutawasaidia watoto wetu kuwa na akili ya kutafuta elimu na mali hata baada ya wazazi wao kuwa hapo duniani,kwani tumeona watu wengi wanawashia watoto mali lakini mali hizo zinatumiwa na watu wengine na watoto wanazidi kuteseka .

Alisema kwamba familia nyingi zimekuwa zitafuta mali bila kuwekeze kwa elimu ya watoto wao na mwisho wa siku watoto wanakosa elimu na mali walizoziacha kwani wanadhulumiwa na wale waliwaacha kusimamia mali hizo .

Mwassa alisema kwamba iwapo wazazi watawaachia elimu watoto wao ni vizuri na hakuna mtu wa kudhurumu elimu hiyo zaidi ya mtoto huyo kuitumia kwa maufaa yake na taifa kwa ujumla .

Alisema kwamba hakuna mtu  ambaye hajui umuhimu wa elimu kwa maana hiyo kila mtoto anatakiwa kupata elimu iliyobora kwa ajili  ya kukabiliana na soko la ajira.

Hata hivyo mkuu huyo wa mkaow a Tabora alifanikisha kuongoza harambee na kuichangia kiasi cha shilingi milioni 25,fedha zilizopatikana zitasaidia kukamilisha ofisi na madarasa ya wanafunzi .

Katika mahafali hayo watoto 42 wa eli mu wa hawali walipatiwa vyeti kwa ajili ya kujiunga na darasa la kwanza mwakani.

Awali shekhe wa mkoa wa Tabora Shabani Salum aliwataka wakazi wa mkoa wa tabora kuwekeza mkoani hapa tofauti  na watu wengine ambao wanawekeza katika mkoa wanayotoka .

Alisema kwamba imekumekuwe[po kasumba ya baadhi ya watu hasa wa mkoa huu kushindwa kuwekeza katika mkoa wao na kuwekeza katika mikoa mingine ,aliomgeza kuwekeza huo sio tatizo bali na msisahua kwenu.


Mwisho



No comments:

Post a Comment