SIKU 16 ZA
KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA
MAZUNGUMZO
NA WAANDISHI WA HABARI (PRESS CONFERENCE)
IJUMAA, TAREHE 23 NOVEMBA, 2012
MAHALI: UKUMBI WA MAKUMBUSHO YA TAIFA
Siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia ni kampeni
kabambe ya kimataifa inayoongozwa na Kituo cha Kimataifa cha Wanawake katika
Uongozi “Women’s Global Leadership” tokea mwaka 1991.
Chimbuko:
Chimbuko la Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia ni mauaji ya kinyama ya wadada wa
Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominika mwaka 1960. Kuanzia Novemba 25 mwaka
1991, Umoja wa Mataifa uliitenga siku hii kama
Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake. Maadhimisho haya
yanafikia kilele tarehe 10 Desemba ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Kuadhimisha
Tamko Rasmi la Haki za Binadamu, ikiwa ni ishara ya kuhusisha ukatili
dhidi ya wanawake na haki za binadamu na vile vile kutia msisitizo kwamba
ukatili kama huu ni uvunjwaji wa haki za
binadamu. Siku hizi 16 pia hutoa mwanga
juu ya siku zingine muhimu kama Novemba 29 ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Watetezi
wa Haki za Binadamu, Desemba 1 ni Siku ya UKIMWI Duniani, Desemba 6 ni siku ya
kukumbuka mauaji ya kikatili ya Montreal
ya mwaka 1989, ambapo (Wanawake 14 waliuawa na mtu aliyekuwa anawachukia
wanawake).
Siku hizi 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia zimekuwa
zikitumika na wadau ulimwenguni kote kama
mbinu mahsusi za kutoa wito kwa jamii ili kumaliza aina zote za ukatili wa kijinsia kwa kufanya
yafuatayo:-
·
Kujenga uelewa
kuhusu ukatili wa kijinsia kama uvunjwaji wa
haki za binadamu kijamii, kitaifa, kikanda na kimataifa.
·
Kuimarisha kazi
za kupinga ukatili wa kijinsia katika ngazi za chini na kujenga daraja kati ya
kazi za maeneo mbalimbali yanayoshughulikia ukatili dhidi ya wanawake.
·
Njia ya
kubadilishana taarifa na uzoefu katika kuzuia na kupambana na ukatili dhidi ya wanawake kati ya wadau.
·
Njia ya
kuonyesha mshikamano ulimwenguni kote kupinga ukatili wa kijinsia.
·
Kama chombo cha
kutumia kupaza sauti ili wadau wote
waweze kutekeleza wajibu wao katika kupiga vita ukatili wa kijinsia.
Kila mwaka kumekuwa na kauli mbiu kuhusiana na
ukatili dhidi ya wanawake.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “FUNGUKA: KEMEA UKATILI DHIDI YA
WANAWAKE. SOTE TUWAJIBIKE”. Kwa
mwaka huu kauli mbiu inasisitiza kuchukua hatua kwa kukemea ukatili dhidi ya
wanawake. Taifa likiwa limejaa vitendo
vya ukatili wa kijinsia kwa makundi fulani ya watu hususan wanawake taifa hilo linabaki kuwa taifa
lisilokuwa na mshikamano na amani, miongoni mwa wananchi wake. Hivyo basi
hatuna budi sote kama jamii kukemea jambo hilo
la ukatili ili kuweza kudumisha mshikamano, amani na maendeleo.
Vitendo vya ukatili wa kijinsia vimekuwa vikiongezeka
kwa kasi kubwa, mathalani takwimu za utafiti uliofanywa na WiLDAF mwaka 2012
kwenye magazeti zilionyesha kwamba
taarifa 6,001 za ukatili ziliripotiwa
kwenye magazeti ikilinganisha na 3,542 za mwaka 2011.
Matokeo ya utafiti uliofanywa na Idara ya Taifa ya Takwimu
ya mwaka 2010 inaonyesha kwamba;
§
Asilimia
39 ya wanawake wanaafiki kwamba mume ana
haki ya kumpiga mkewe iwapo mke atajibishana naye.
§
Asilimia
37 ya wanawake waliohojiwa wanaafiki kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe kwa
sababu ya kuondoka nyumbani bila ya kumuaga mumewe.
§
Asilimia
40 ya wanawake wanakubali kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe pale mwanamke
anapozembea kuangalia watoto.
§
Asilimia
30 ya wanawake wanakubali kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe iwapo atakataa
kufanya tendo la ndoa.
§
Asilimia
18 ya wanawake wanaafiki kwamba mume ana
haki ya kumpiga mkewe ikiwa ataunguza chakula.
§
Asilimia
53 ya wanawake wanaafiki kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe kwa sababu
nyingine yeyote ile.
Ukatili wa Kijinsia umekuwa ukifanywa kwa njia mbali mbali kama
vipigo, ukeketaji, ubakaji, mauaji ya wanawake na watoto wa kike, mauaji ya
Albino, kurithi wajane, ukatili nyumbani n.k. Ukatili una athari mbaya kwa wanawake, kwani huathiri afya zao kimwili
na kisaikolojia na hivyo hupelekea
kudidimiza maendeleo yao na ya taifa kwa ujumla wake. Aidha ukatili wa kijinsia husababisha msongo
wa mawazo, kutokujiamini, ulemavu wa kudumu na wakati mwingine kifo. Bado tunaamini mabadiliko chanya yanaweza kutokea na hivyo kuwa na jamii
isiyokuwa na ukatili wa kijinsia. Changamoto
kama mfumo dume, mila na desturi zilizopitwa na wakati, umaskini pamoja na
elimu duni ni lazima tupambane nazo vilivyo ili kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Ni lazima tuzingatie kwamba hata kama sisi wenyewe siyo wahanga wa
ukatili, tuna wajibu wa kutokaa kimya tunapowaona jirani, marafiki na watu
tunaowafahamu wanafanyiwa ukatili wa kijinsia.
Kutokana na hali hii, Tanzania
kama nchi nyingi duniani imekuwa ni sehemu ya kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili
wa Kijinsia.
Kwa hapa Tanzania, kampeni ya
Siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia, inaratiwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo
Afrika (WiLDAF) kwa shirikiana na Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia
(MKUKI) pamoja na Kikosi kazi cha maandalizi ya Siku 16 ambacho kinajumuisha pamoja na idara mbali mbali za serikali zikiwamo
wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wizara ya Mambo ya Ndani,
Mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania. Kampeni
hii inafanyika katika kanda mbalimbali na kuzinduliwa rasmi kote nchini tarehe
26/11/2012.
Ifuatayo ni orodha ya kanda mbalimbali na waratibu wake nchi nzima. Kanda ya
Mashariki (Dar es salaam, Morogoro na Pwani)
inaratibiwa na WiLDAF, Kanda ya Kati (Dodoma na Singida) inaratibiwa na Mtandao wa Kutokomeza
Ukeketaji wa Wanawake (AFNET), Kanda ya Magharibi (Kigoma na Tabora)
inaratibiwa na Jeshi la Polisi, chini ya mtandao wa wanawake polisi (TPFNet)Kanda
ya Kaskazini (Kilimanjaro, Manyara, Tanga na Arusha) inaratibiwa na Shirika
linalojihusisha na Ukeketaji (NAFGEM), Kanda ya ziwa (Mwanza, Shinyanga na
Mara) inaratibiwa na shirika la KIVULINI pamoja na Action Based Community
Foundation (ABC Foundation) na Kanda ya Kusini (Mtwara, Lindi, Mbeya, Iringa na
Songea) inaratibiwa na Kituo cha Wasaidizi wa Msaada wa Kisheria Iringa.
Katika kanda ya Mashariki yaani Dar es salaam,
Pwani na Morogoro Shughuli zifuatazo zitafanyika;
Uzinduzi wa Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Utafanyika tarehe 26 Novemba, 2012, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee (VIP Hall),
mgeni rasmi atakuwa ni NaibuWaziri wa Sheria
na Katiba Mheshimiwa Angelah Kairuki. Katika siku hii mada mbalimbali kuhusu
ukatili wa kijinsia zitajadiliwa zikiwamo :-
·
Fomu Mpya ya
Polisi Namba 3
·
Ripoti ya
Utafiti Kuhusu Ukaitli wa Kijinsia na Makosa ya kujamiiana kulingana na Sheria
ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16.
·
Dhana ya ukatili
wa kijinsia na Dhima ya Jeshi la Polisi kuitokomeza.
·
Hali halisi ya huduma
za afya kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.
Aidha, Fomu ya Polisi namba 3 (Mpya) itazinduliwa
rasmi. Aidha msafara wa kupinga ukatili wa kijinsia
utazinduliwa. Msafara huu uaanza Dar es salaam siku ya tarehe 26 Novemba na
kwenda Kilimanjaro, Singida, Shinyanga, Mwanza na kuishia Mara (Tarime), wilabya
ambayo imekubuhu kwenye suala la ukeketaji wa wanawake na watoto wa kike.
Aidha, katika siku hii ya uzinduzi Msaada wa Kisheria
na maonyesho mbali mbali pamoja na elimu ya afya vitatolewa bila malipo.
Kutakuwa na shughuli mbalimbali za kampeni kupinga
ukatili wa kijinsia zitakazofanywa na Mashirika na Mtandao wa Kupambana na
Ukatili wa Kijinsia. Baada ya uzinduzi wa tarehe 26 Mashirika yatakayokuwa na
shughuli katika siku 16 ni pamoja na;
·
27/11/2012 Jeshi la Polisi
Katika harakati ya kupunguza uhalifu Polisi
watatembelea kila nyumba – Dar es
salaam kuhamasisha jamii kukemea ukatili wa kijinsia
na ukatili dhidi ya watoto, kubandika matangazo dhidi ya ukatili wa kijinsia kwenye magari n.k.
·
28/11/2012 Jeshi la Polisi
Katika harakati ya kupunguza uhalifu Polisi
watatembelea kila nyumba – Dar es
salaam kuhamasisha jamii kukemea ukatili wa kijinsia
na ukatili dhidi ya watoto, kubandika matangazo dhidi ya ukatili wa kijinsia
kwenye magari, n.k.
·
28/11/2012 World Vision
Watakuwa na Kampeni kuhusu Afya ya Mtoto sasa,
Mgeni rasmi- Waziri Mkuu.
Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro Kempinski.
·
29/11/2012 TAWLA
Diamond Jubilee
Mjadala kuhusu Ukatili wa Kijinsia
Mgeni Rasmi Dk. Asha Rose Migiro.
·
30/11/2012 Jeshi la Polisi
Katika harakati ya kupunguza uhalifu Polisi
watatembelea kila nyumba katika jiji la Dar es salaam kuhamasisha jamii ili kukemea ukatili wa kijinsia na ukatili
dhidi ya watoto, kubandika matangazo dhidi ya ukatili wa kijinsia kwenye magari
n.k.
· 28-30/11/2012 WiLDAF
Kusimamia na
kufuatilia msafara wa kupiga vita
ukatili wa kijinsia
·
3-4/12/2013 Jeshi la Polisi
Katika harakati ya kupunguza uhalifu Polisi
watatembelea kila nyumba – Dar es
salaam kuhamasisha jamii kukemea ukatili wa kijinsia
na ukatili dhidi ya watoto.
·
5/12/2013 Equality
for Growth (EFG)
Uzinduzi wa Kupiga vita ukatili wa kijinsia katika wilaya
ya Ilala watatembelea masoko mbalimbali ya wilaya hii.
·
6/12/2013 EngenderHealth/CHAMPION
Project.
Uzinduzi wa Kupiga vita ukatili wa kijinsia mkoa wa
Iringa. Watatembelea vijiji 20 vya Iringa.
·
8/12/2013 Children Dignity Forum CDF
Watatoa msaada wa kisheria Mkoa wa Pwani, pia
wataendesha shughuli mbalimbali kupiga vita ukeketaji katika Mkoa wa Mara, Wilaya ya Tarime.
·
10/12/2013 Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
Kwa kushirikiana na wadau wengi wataratibu
maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu
tarehe 10/12/2011 hapa hapa Dar es salaam na kuhitimisha maadhimisho ya Siku 16
za Kupinga Ukatili wa Kijinsia.
Mwisho kabisa ninapenda kutoa wito kwa jamii kwamba
kila mmoja wetu anaweza kukemea na kuchukua hatua dhidi ya ukatili dhidi ya
wanawake. Dhamiria kutofanya ukatili, zungumza wazi kuhusu ukatili wa kijinsia,
saidia wanawake na watoto wanaofanyiwa ukatili, jiunge na makundi yanayokemea
ukatili. Kwa pamoja tuzinduke, tukemee
ukatili dhidi ya wanawake, sote tunawajibika.
Ahsanteni kwa
kunisikiliza.
Imetolewa na:-
Dk. Judith N. Odunga
MRATIBU KITAIFA
Shirika la
Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF)
S. L. P 76215,
DAR ES SALAAM,
SIMU: 2701995,
Barua
pepe: wildaf_tanzania@yahoo.com
No comments:
Post a Comment