Nikiianza
safari yangu ya kurejea Bandari salama Dar es salaam kutoka mkoani
Katavi ambako nilihudhuria uzinduzi wa mkoa huo, nimepitia barabara ya
Mpanda mkoani Katavi-Sumbawanga mkoani Rukwa mpaka Tunduma mkoani
Mbeya, ambapo nimejionea mwenyewe na kupata taswira za maeneo
mbalimbali ambayo ujenzi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga-Mpanda
unaoendelea kwa kiwango cha lami na kufurahishwa na hatua iliyofikiwa
hasa kwa upande wa Sumbawanga -Tunduma.
Ni jambo la kufurahisha kwamba
muda mfupi ujao kero ya Usafiri katika mikoa ya Rukwa na Katavi itakuwa
ni historia tu, jambo ambalo linafungua fursa mbalimbali za kimaendeleo
na kiuchumi katika mikoa hiyo iliyokuwa katika mdororo wa kiuchumi kwa
muda mrefu kutokana na miundombinu ya barabara kuwa katika hali mbaya.
Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania
inaonyesha mwanga wa maendelea katika ukanda huo kutokana na hatua
inayopigwa katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, ni wazi kwamba
sasa hali ya maisha ya wakazi wa mikoa hiyo itaboreka zaidi kutokana na
kufunguka kwa fursa za kimaendeleo kwa wakazi wa mikoa hiyo Asante
Serikali kwa kuliona hilo na kulivalia njuga.
Taarifa zaidi ya makampuni
yanayojenga barabara hizo, kilomita zake na gharama ya ujenzi huo
utaiona chini ya Taswira hizi endelea kushuka chini mdau.
17.5.1. SEHEMU YA SUMBAWANGA – LAELA (95.31KM)
Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya
Aarsleff-BAM International Joint Venture V.O.F Kutoka Denmark na
Uholanzi kwa gharama ya dola za Kimarekani 97 Milioni chini ya Mhandisi
Mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufarasa.
Maendeleo ya jumla ya mradi hadi
kufikia tarehe 31 Octoba, 2012 yalikuwa yamefikia 49.9% ya kazi zote
zilizopangwa. Kwa ujumla mradi unaendelea vizuri na ulipangwa kwisha 31
Januari 2013 ingawa majadiliano kuhusu kuongeza muda wa kumaliza kazi
bado yanaendelea.
17.5.2. SEHEMU YA LAELA – IKANA (64.2KM)
Sehemu hii inajengwa na Kampuni ya China New Era
International Engineering Corporation kutoka China kwa gharama ya Sh.
bilioni 76.1 chini ya Mhandisi Mshauri Egis BCEOM International kutoka
Ufarasa na unategemea kukamilika 31 Mei 2013.
Maendeleo ya jumla ya mradi hadi
31 Octoba, 2012 yalikuwa yamefikia 64% ya kazi zote zilizopangwa. Kwa
ujumla mradi unaendelea vizuri.
17.5.3. SEHEMU YA IKANA – TUNDUMA (63.7KM)
Sehemu hii inajegwa na Kampuni
ya Consolidated Contractors Group S. A (Offshore) (CCC) kutoka Ugiriki
chini ya Mhandisi Mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufarasa kwa
gharama ya Sh. bilioni 82.5. Maendeleo ya jumla ya mradi hadi sasa
yamefikia 43% ya kazi zote zilizopangwa. Mradi huu ulitegemewa
kukamilika tarehe 9 Septemba 2012, hata hivyo muda wa kumaliza kazi
uliongezwa hadi tarehe 31 May 2013.
17.6. SUMBAWANGA – NAMANYERE – MPANDA NA KIZI – KIBAONI (245KM)
17.6.1. SEHEMU YA SUMBAWANGA – KANAZI (75KM)
Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya
Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China chini ya
Mhandisi Mshauri Nicholas O’Dwyer and Company Limited kutoka Ireland
akishirikiana na Apex Engineering Ltd. kutoka Tanzania kwa gharama ya
Sh. bilioni 78.8.
Maendeleo ya jumla ya mradi hadi
kufikia tarehe 31 Octoba, 2012 yalikuwa 23.6% ya kazi zote
zilizopangwa. Kasi ya maendeleo ya kazi inasuasua kwa madai kuwa
mkandarasi hajalipwa kiasi chote anachodai. Mradi huu ulitegemewa
kukamilika tarehe 15 Desemba, 2012, hata hivyo muda wa kumaliza kazi
bado unajadiliwa.
17.6.2. SEHEMU YA KANAZI – KIZI – KIBAONI (76.6KM)
Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya
China Hunan Construction Engineering Group Corporation kutoka China,
chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O’Dwyer and Company Limited kutoka
Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd. kutoka Tanzania, kwa
gharama ya Sh. 82.84 bilioni.
Maendeleo ya jumla ya mradi hadi
tarehe 31 Octoba, 2012 yalikuwa 30% ya kazi zote zilizopangwa.
Mkandarasi anaendelea na kazi ingawa kwa kasi ndogo kwa madai ya
kuchelewa kulipwa. Mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 15 Desemba,
2012, lakini haitawezekana. Hivyo muda wa kumaliza bado unajadiliwa.
17.7. SUMBAWANGA – MATAI – KASANGA PORT (112KM)
Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya
China Railway 15 Bureau Group Corporation (CR15G)/ Newcentry Company
Ltd. chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O’Dwyer and Company Limited
kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd, kutoka
Tanzania. Gharama ya Mradi ni Sh. 133.30 bilioni.
Maendeleo ya jumla ya mradi hadi
kufika tarehe 31 Octoba, 2012 yalikuwa 28% ya kazi zote zilizopangwa.
Mradi huu unatekelezwa kwa mkataba wa Usanifu na Ujenzi (Design and
Build Contract). Kwa sasa kazi zinaendelea vizuri baada ya kusuasua
siku za nyuma. Mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 13 Januari, 2013
lakini itabidi muda wa utekelezaji kuongezeka kutokana sababu
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment