Mmoja kati ya vijana
akicheza”Break Dance”wakati wa uzinduzi rasmi wa kinywaji kipya
kisichokuwa na
kilevi cha Alvaro kinachotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti
Breweries
LTD.
Baadhi ya vijana
walioshiriki
katika uzinduzi wa kinywaji kisichokuwa na kilevi cha Alvaro
kinachotengenezwa
na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries wakionesha umahiri wao wa
kucheza
katika uzinduzi rasmi wa kinywaji hicho jijini Dar es Salaam hapo jana.
Warembo walioshiriki katika
uzinduzi rasmi wa kinywaji kipya kisichokuwa na kilevi cha aina ya
Alvaro
kinachotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries
LTD,Wakionesha
umahiri wao wa kucheza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es
Salaam.
Vijana walioshiriki katika
uzinduzi wa kinywaji kisichokuwa na kilevi cha Alvaro kinachotengenezwa
na
Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries,wakigonganisha chupa zao kuashiria
ishara
ya uzinduzi rasmi wa kinywaji hicho hapo jana jijini Da es Salaam.
---
NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti imezindua kinywaji kipya kisicho
na
kilevi kinachoitwa Alvaro ambacho kimekuwa kikizalishwa muda mrefu
katika nchi
nyingine za Afrika Mashariki.
Katika uzinduzi wa aina yake uliofanyika mwishoni mwa wiki
jijin
Dar es Salaam, Meneja wa Kinywaji hicho Anita Msangi alisema kinywaji
hicho
kitakidhi wateja wanaotumia vinywaji visivyo na kilevi
Uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika katika kumbi za Mlimani
City na Quality Plaza jijini, Dar es Salaam, ulivutia watu kutoka
matabaka
mbalimbali ambao walionekana kufuruhishwa na ladha ya kinywaji hicho.
Akizungumza katika sherehe hizo, Bw. Njowoka aliahidi
watumiaji
wa kinywaji hicho na vingine vinavyotengezwa na kampuni ya Serengeti
kuwa
kampuni yake imejipanga kuona kuwa wateja wanapata bidhaa bora zenye
viwango
vya hali ya juu vinavyostahili na kukidhi matakwa ya wateja wake.
Pamoja na wageni wengi waliofika kwenye uzinduzi huo, sherehe
za
kuzindua kinywaji hicho pia zilipambwa na vikundi mbalimbali vya vijana
ambavyo
vilionesha uweso mkubwa katika sanaa ya muziki pamoja na kucheza dansi.
Kinywaji cha Alvaro kimekua kikizalishwa kwa muda mrefu katika
nchi za Uganda na Kenya kupitia kampuni mama ya kiwanda cha kutengzeneza
bia
cha Serengeti iitwayo East African Breweries Limited.
No comments:
Post a Comment