Na
Lucas Raphael,Tabora
Watu
sita walio vunja ofisi na kuiba mitihani ya
kidato cha pili katika
shule
ya sekondari Bukene wilayani Nzega Mkoani Tabora wamefikishwa mahakamani jana
na kwa kujibu tuhuma hizo zinazo wakabili.
Watuhumiwa
hao sita wakiwepo na wanafunzi watatu walifikishwa mbele ya mahakama ya hakimu
mkazi wilaya ya Nzega Nov,12 mwaka huu kwa tuhuma za kuvunja ofisi ya mwalim
mkuu na kuiba mitihani mitatu ya taifa ya kidato cha pili ambayo inayoendelea
kufanywa na wanafunzi wa kidato hicho sehemu mbalimbali hapa nchini.
Mwendesha
mashitaka wa polisi Merito Ukongoji akisoma mashitaka hayo mbele ya hakim mkazi
Joseph Ngomero kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa kuvunja ofisi ya mwalimu
mkuu wa shule ya sekondari Bukene
iliyokuwa ikihifadhi mitihani hiyo Nov 9 mwaka huu majira ya saa 2 usiku hadi
saa 6 usiku.
Ukongoji
aliwataja watuhumiwa hao sita wakiwepo na wanafunzi watatu kuwa ni charles
fabiani(48) ambaye alikuwa mlinzi wa ofisi ya mwalim mkuu,Thabiti saidi(20)
mkazi wa Bukene,Rashidi shaibu(18) m kazi wa bukene.
Katika
tuhuma hiyo wanafunzi wakiwa ni salehe matongoro(17) mwanafunzi kidato cha tatu
shule ya sekondari kili, Matius Daudi (16)pamoja na Abdalallha Hamis(15) ni
wanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Bukene.
Kesi
hiyo ikisikilizwa kwa Malaya ya kwanza
imeahilishwa mpaka Nov 19 mwaka huu itakapo sikilizwa kwa mala ya pili.
Mitihani
iliyoibiwa na watuhumiwa hao ni mitatu ikiwepo na mtihani wa Physcs,Biology na
chemistry hata hivyo kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya
ya nzega Kyuza kitundu alisema kuwa udhibiti mkali ulifanyika kuhakikisha
mitihani hiyo haikufika kwa shule jirani zilizoko karibu na tukio hilo lilipo
tokea.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment