Wednesday, November 14, 2012

WIKI YA KIMATAIFA YA UJASIRIAMALI YAZINDULIWA JIJINI DAR SAMBAMBA NA MAFUNZO KWA VITENDO


Chief Technical Advisor Youth Entrepreneurship Facility and WED -ILO Bw. Jealous Chirove akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Kimataifa ya Wajasiriamali uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amesema vijana lazima wawe na moyo wa kujituma na kuhakikisha wanapanua wigo wa kujiajiri wenyewe na kuondokana na fikra za kuajiriwa peke yake.
Aliongeza kuwa ujasiriamali katika nchini kama Tanzania ni mkombozi wa pekee katika tatizo la ajira hasa kwa vijana kwa kujiendeleza na mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali kama njia pekee ya kujiajiri wenyewe.
Mwenyekiti wa Shirika Lisilo la Kiserikali la ZAYEE (Zanzibar Association for Youth Education and Empowerment) Bw. Masoud Salim Mohamed ambao ndio waandaaji wa maadhimisho ya wiki ya wajasiriamali inayoendea jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Shirika Lisilo la Kiserikali la ZAYEE (Zanzibar Association for Youth Education and Empowerment) Fatma Mabrouk Khamis akielezea jinsi alivyovutiwa kufanya maadhimisho ya Wiki ya Kimataifa ya Wajasiriamali hapa Tanzania ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kuona yanavyofanyika nchini Marekani alikokwenda kujifunza juu ya ujasiriamali.
Mwenyekiti na Mwanzilishi wa East African Speakers Bureau Limited (EASB) Paul Mashauri akizungumzia umuhimu wa kukuza mtandao wa vijana wajasirimali nchini ili kupanua wigo wa mawasiliano miongoni mwao katika moja ya njia ya kukuza vipaji na mawasiliano ya kirafiki.
Mratibu Kitaifa Mradi wa Maendeleo ya Ujasiriamali kwa Wanawake (WED) Bi. Noreen Toroka akitoa changamoto kwa mabinti waliohudhuria semina hiyo kutokuwa na uwoga wa kuchangia mada na kuuliza maswali na vile vile kujiamini pia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Professional Approach Group Modesta Mahiga akitoa nasaha zake kwa vijana mbalimbali kuhusu ujasiriamali faida na changamoto zake wakati wa maadhimisho ya wiki ya ujasiriamali hapa nchini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Relim Entertaiment, Bi. Emelda Mwamanga Mtunga akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya ujasiriamali ambapo alitumia nafasi hiyo kuelezea uzoefu na changamoto za ujasirimali nchini.
Mshehereshaji wa Wiki ya Kimataifa ya Wajasiriamali (GEW) Bw. Austin Makani akitambulisha baadhi ya Wafanyakazi wa ILO (hawapo pichani).
Baadhi ya Wafanyakazi vijana wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) wakitambulishwa wakati wa semina ya Ujasiriamali inayohusisha asilimia kubwa ya vijana jijini.
Pichani Juu na Chini ni baadhi wa washiriki waliohudhuria wiki ya Ujasiriamali nchini. Mafunzo hayo yameandaliwa na Shirika la Kazi Duniani ILO kwa kushirikirikana na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya ZAYEE.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na washiriki wa wiki ya Wajasiriamali nchini iliyozinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam itakayodumu kwa muda wa wiki nzima nchini.

No comments:

Post a Comment