Rais Jakaya Kikwete akimuapisha Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Winfrida Korosso mara baada ikulu jijini Dar es Salaam, leo. (Picha na Habari Mseto Blog)
Rais Jakaya Kikwete
akimkabidhi vitendea kazi Katibu wa Tume
ya Kurekebisha Sheria, Winfrida Korosso mara baada ya kuapishwa kuwa katibu wa
tume hiyo, Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanafamilia
(Picha na Habari Mseto Blog)
DAR ES SALAAM, Tanzania
RAIS Jakaya Kikwete, leo amewaapisha majaji wa mahakama
kuu ya rufani, wajumbe wa tume ya uchaguzi na katibu wa tume ya kurekebisha
sheria, hafla iliyofanyika katika makazi ya Rais Ikulu jijini Dar esSalaam.
Majaji walioapishwa
kufanya kazi katika mahakama ya rufani ni Bethel Makani na Ibrahim
Khamis Jumaa,wakati Jaji mstaafu John Mkwawa ameapishwa kuwa mjumbe wa tume ya
taifa ya uchaguzi, huku Winnfrida Koroso, akiapishwa kuwa mjumbe wa tume ya
kurekebisha sheria.
Wakizungumza baada ya kuapishwa kushika nafasi hizo wateule
hao walisema watahakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na moyo wa kujitolea
kuhakikisha haki inatendeka katika nafasi walizo nazo.
Makani alisema katika nafasi yake hiyo mpya anayoenda
kufanyia kazi kuna changamoto nyingi ikiwemo wananchi kudhani suala la
kucheleweshwa au kuahirishwa kwa kesi mbalimbali kunasababishwa na mahakimu
pamoja na majaji.
“Ni mara chache hakimu kuahirisha kesi kama kutakuwa kila
kitu kimekamilika nah ii hali ya kuchelewa kwa kesi ina mzunguko mkubwa ikiwa
ni pamoja na wananchi wenyewe kusdhindwa kutoa ushirikiano na idara husikia
katika kupata ukweli wa kufanyia uamuzi”alisema Makani.
Kwaq Upande wake jaji John Mkwawa alisema katika nafasi
anayoenda kuhudumu changamoto zilizopo ni pamoja na kufanyia marekebisho
daftari la kudumu la wapiga kura iuli liendane na mahitaji ya sasa ya
watanzania.
Alisema changamoto nyingine ni ucheleweshaji wa matokeo
baada ya uchaguzi na kwamba hali hiyo inatokana na kutokuwepo kwa teknolijia ya
kisasa ya kuweza kufanyia kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment