Wednesday, November 14, 2012

ALBINO WAFARIKI KWA KANSA TABORA



Na Lucas Raphael,Tabora

Zaidi ya watu kumi wenye ulemavu wa ngozi Albino wamefariki dunia kutokana na kansa ya ngozi mkoani Tabora kutika kipindi cha mitatu iliyopita.

Katibu wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi mkoani Tabora  Musa Kabimba amesema kwa mwaka huu 2012 wamefariki dunia watu wanne huku mwaka jana wakifariki watatu na mwaka juzi wamefariki watu sita wenye ulemavu huo.

Kabimba amesema kwamba kansa ya ngozi ni ugonjwa unaowatesa sana albino na hadi sasa jumla ya watu hao wanaugua kansa ni ishirini na tano kati ya albino 920 waliopo mkoani Tabora.

Kabimba ambaye pia ni naibu Katibu mkuu chama cha albino Taifa  amesema kupata kansa ya ngozi kwa albino kunatokana na hali ya maisha ambapo hulazimika kufanya kazi zinazowafanya wangue juani kama ukulima na ufugaji.

Amebainisha ya kwamba ili kuondokana na tatizo hilo ni lazima albino wapewe elimu ili wasikae juani au kijikinga juani pamoja na kuwezzesha kiuchumi ili shughuli zao zisiathiri miili yao.

Kabimba ametoa wito kwa watu wenye mapenzi mema, kuwassidia walemavu wenye ulemavu ngozi aidha kielemu kiuchumi ili wasipate kansa ya ngozi na kufariki mapema.

Mwisho

No comments:

Post a Comment