Thursday, January 3, 2013

Airtel yawazawadia washindi wa mwenzi wa “Amka Millionea” promosheni shilingi million 30


 Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuendesha droo ya mwenzi  wa washindi wa Amka Millionea, Ambapo moja kati ya washindi ni  bw Rickson Richard kutoka Arusha aliyejishindia shillingi million 15. pichani  Katikati ni Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami akifatiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki Elimsu. 
 Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki Elimsu wakitafuta washindi wa mwenzi wa promosheni ya Amka Millionea ambapo Ambapo moja kati ya washindi ni bw Rickson Richard kutoka Arusha ambaye amejishinid kitita cha shillingi million 15.  wakishuhudia ni waandishi wa habari , kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde
Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde akiongea na Mshindi wa Amka Millionea bw Rickson Richard (19) kutoka Arusha  mara baada ya kuibuka kuw mshindi wa shillingi million 15 wa promosheni ya Amka millionea, Katikati ni Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami akifatiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki Elimsu
.............................................
Airtel yawazawadia washindi wa mwenzi wa “Amka Millionea” promosheni shilingi million 30

    Washindi wawili wapatikan, Kila mmoja aondoka na kitita cha shilling million 15
2 January 2013  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo iwatangaza washindi  wa mwenzi wa promosheni “Amka Millionea” wa pesa taslimu  million 30 mara baada ya kuibuka washindi kupitia droo iliyofanyika leo asubuhi ambapo kila moja ameibuka na  kitita cha shilingi milioni 15 pesa taslimu.

Akitangaza washindi hao mara baada ya droo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania  kushiriki na Kushinda fedha taslimu kwa kupiti promosheni yetu hii kabambe ya “Amka Millionea” iliyozinduliwa mwanzoni mwa mwenzi December, mpaka sasa wateja zaidi ya 300 wamejishindia zawadi za pesa taslimu zenye thamani  zaidi ya shilingi million 120.  Promosheni ya Amka millionea inawazawadia wateja wa Airtel  Kila siku , kila wiki na leo tunashuhudia wateja wawili wa mwisho wa mwenzi wakiibuka kuwa washindi wa shilingi million kumi na tano kila mmoja.

Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru, aliongeza Matinde

Akiongea kwanjia ya simu mara baada ya kutangazwa mshindi, Rickson Richard  mkazi wa Arusha na mwanafunzi wa kidato cha tano  katika shule ya Lyamungo high school alisema’ nimefurahi kuibuka mshindi wa milioni 15 wa promosheni ya Amka millionea, pesa hizi ntazitumia katika masomo yangu shule na kumsaidia baba yangu ambaye ndiye aliyenipa pesa za kuchezea promosheni hii.  nawaambia watanzania  ­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­waamini wanaweza kushinda na kujiunga kwani mimi nimecheza na nimeshinda kwa Bahati nao pia wananafasi ya kujishindia kama mimi.

Tunapenda kuwajulisha kuwa promosheni hii bado inaendelea na kukupa nafasi ya kuwa mmoja kati ya washindi wa mamilioni ya fedha  kila siku, kila wiki, kila mwezi  au mshinid wa zawadi kubwa moja itatolewa mwisho wa promosheni. 

Ili mteja aweze kushiriki inabidi atume neno WIN/SHINDA kwenda namba 15595 bure , Baada kujiunga mteja atakuwa atapata ujumbe kutoka 15656 na kupata maswali ambayo atajibu na akipata sahihi atapata ponti 20 akikosea atapata ponti 10. Na kwakila ujumbe atakaotuma atatozwa kiasi cha shilingi 350 pamoja na kodi.

No comments:

Post a Comment