Sunday, January 6, 2013

DK SHEIN AFUNGUA WA JENGO LA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA,TUNGUU


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,  akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kati Vuai Mwinyi,alipowasili katika shere za Ufunguzi wa Jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,liliopo Tunguu,Wilaya ya Kati Unguja,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya ufunguzi wa jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja jana,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Utumumishi wa Umma na Utawala Bora Haji
Omar Kheir.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo  cha Utumishi wa Umma,(IPA) Harusi Masheko Ali,alipotembelea madarasa ya kusomea,baada ya ufunguzi rasmi wa Jengo la Chuo hicho uliofanyika jana Tunguu, Wilaya ya Unguja, katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akifuatana na   Waziri wa Utumumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheir,(kushoto) pamoja na Viongozi wengine baada ua kulifungua  jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja jana,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Baadhi ya   Viongozi na Wananchi walioalikwa katika sherehe za Ufunguzi wa  jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,zilizofayika jana huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja, wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Rais wa Zanzibar,alipokuwa akitoa hutuba yake katika kusherehekea shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baadhi ya   Viongozi na Wananchi walioalikwa katika sherehe za Ufunguzi wa  jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,zilizofayika jana huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja, wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Rais wa Zanzibar,alipokuwa akitoa hutuba yake katika kusherehekea shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akiwahutubia Wananchi, katika sherehe za ufunguzi wa  jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja jana,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Maalim Abdalla Suleiman,(wa pili Kulia) na   Waziri wa Utumumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheir,(kushoto) .Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
…………………………………………………….
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein ametowa wito wa Taasisi za Serikali na Taasisi Binafsi kukitumia Chuo cha Utawala wa Umma ili kuwajengea uwezo wafanyakazi wao kwa manufaa ya Taifa. 

Amesema kuwa Chuo hicho kitaweza kuwajengea uwezo ujuzi ubunifu uwandilifu na kuweza kuwa watumishi bora wa taifa na jamii kwa ujumla . Hayo aliyasema leo huko  Tunguu Mkoa wa kusini Unguja  wakati alipokuwa akifungua Jengo Jipya la Chuo cha Utawala wa Umma  ikiwa ni miongoni mwa  shamra shamra  za sherehe ya miaka 49 ya  Mapinduzi ya Zanzibar .
Amesema kuwa madhumuni makubwa  yakujenga vyuo  hivyo ni kuleta mabadiliko yenye lengo la kupata ustawi bora wa maisha kwa Wazanzibar  na kuwa na wafanyakazi wenye taaluma inayostahiki .
 
 Pia  amesema kuwa chuo hicho kitaweza kutowa wanafunzi waliobora wenye misingi imara ya utawala bora na kuweza kujua haki na majukumu ya kazi zao. Aidha Dkt Shein ameuomba uwongozi kujitahidi kuwa na wakufunzi ambao wataofundisha katika chuo hicho kuwa na sifa zinazokubalika ili chuo hicho kiweze kutoa wanafunzi bora .
 
 Halikadhalika aliutaka uwongozi  kuwajengea mazingira mazuri wakufunzi wa chuo hicho ili wasiweze kuvunjika nguvu katika utendaji wa kazi zao . Jumla ya shilling bilioni 1milioni mia moja na saba tayari zimeshatumika  mpaka sasa  kwa ajili ya Ujenzi huo na hivi sasa zinahitajika shilingi milioni elfu 3 kuweza kuinua Jengo hilo kuwa la ghorofa moja. Jengo la chuo hicho linatarajiwa kuwa na sehemu nyengine mbali mbali  zikiwemo za kuegesha magari,mkahawa,  mabweni  na uwanja wa michezo .

No comments:

Post a Comment