Friday, January 11, 2013

HAKUNA MTANZANIA ATAYEKUFA KWA NJAA -JK

 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya watoto wanaoishi katika kijiji cha Igombe manispaa ya Tabora wakati wa ziara yake hapa mkoani Tabora.


Na Lucas Raphael,Tabora

RAIS wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete amewatoa hofu watanzania na kusema kwamba hakuna mtanzania yoyote atakaekufa kwa njaa japo maeneo mengi ya nchi yamekuwa yakilalamikia tatizo la kuwepo kwa njaa kwa baadhi ya mikoa na wilaya.
 
Kauli hiyo aliitoa juzi wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya chipukizi mjini Tabora wakati wa ziara yake mkoani hapa.
 
Alisema kwamba kutokana na tatizo la njaa kwa baadhi ya mikoa serikali ipo tayari kuhakikisha hakuna mwananchi ama mtanzania atakaye kufa kutokana na janga hilo.
 
Alisema kwamba tayari srikali imejipanga kuhakikisha kila mtu anapata chakula cha msaada kupitia kamati za mahafa za wilaya kata na mkoa kwa ajili ya kupatiwa chakula hicho .
 
Dkt Kikwete alisisitiza kwamba hifadhi za chakula zilizopo katika mikoa ya shinyanga kwa ukanda huu inachakula cha kutosha kwa ajili ya wananchi wa mikao ya ukanda huu.
 
Hata hivyo alisema kwamba kama chakula kitakwisha kwenye magahala yan hifadhi za taifa serikali ipo tayari kuangiza chakula hicho hata nje ya nchi ili kuakikisha kuna mtu anayejkufa kwa kukosa chakula .
 
Alisema kwamba licha ya ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa tayari kimefanya  tathimini ya mahitaji ya chakula kwa baadhi ya mikoa na wilaya hapa nchini na katika maghala ya hifadhi ya chakula na kuonyesha kuwa  bado kipo na chakutosha kwa mikoa ambayo imeomba chakula kwa ajili ya wananchi wake .
 
Rais kiwete akizungumzia swala la ukimwi alisema bado maambukizi ya ukimwi yanatishia maisha ya watanzania wengi na kuwataka wanatanzia watumia kinga kwa ajili ya kufanya tendo hilo.
 
Alisema kwamba kitendo cha wananchi wengi nchini kupata maambukizi ya ukimwi na ukimwi imekuwa si cha dharula bali ni chakujitakia na cha makusudi kwani kabla ya kwenda kwenye haadi lazima kupanga wapi mkutane na kufanya kitendo hicho.
 
Alisema kwamba sasa kabla ya kufanya inabidi kila mtu hatafute kinga na nani haje nayo ili kuwaza kujikinga na mambakizi hayo ya ukimwi .
 
“jamani hali ya maambukizi ya ukimwi nchini yanatisha lakini basi tumieni kinga ili maambukizi hayo yasiongezeke kwani kitendo hicho kipangwa muda na saa sasa nini kinashindikana kununua kinga ili kuwaze kujikinga wote na maambukizo hayo”.alihoji rais kikwete.
 
Alisema kwamba katika kipindi cha januari hadi septemba mwaka jana mkoa wa tabora jumla ya watu 41,032 walipimwa ,kati hao wanaume 19 ,531 na wanawake 21,591.
 
Alisema kuwa watu 3,136 walikutwa na maambukizi ya ukimwi kati yao ni wanaume 1,324,na wananwake 1820sawa na asilimia 7.6 kwa wale waliopima hali hii inaonesha bado maambukizi yapo juu.
 
Dkt kikwete aliendelea kusema kwamba watu 39,659 wanahudhuria klinik na kati ya hao watu 20,486 wanatumia dawa na ARVs ambao ni sawa na asilimia 51.6 .
 
Alisema kwamba kwa hali  hiyo ni mbaya sana hivyo kila mmoja wetu anawajibu mkubwa wakujilinda afya yake .
 
Hata hivyo Rais Jakaya Kikwete  amewahakikishia wananchi wa tarafa ya iloloagulu katika wilaya ya Uyui kuwa swala la wilaya hiyom kuwa na halmashauri mbalin linawezekana ili kupunguza kero kwa wananchi hao.
 
Awali mwenyekiti wa srikali ya kijiji cha ilolagulu ,Ally Magowa alimwambia Rais kwamba wananchi wa kijiji hicho wamekuwa wakitembea umabli mrefu kw ajili ya kupata huduma za kiserikali kutoka hapo hadi Isikizya .

No comments:

Post a Comment