Wednesday, January 2, 2013

TAJIRI AMPIGA RISASI MLALAHOI BAADA YA KUDAIWA 15000 NZEGA



Levis Ndugu akiwa amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mguu wa kushoto kufuatia alikwenda kudai pesa yake  shilingi 15000 baada ya kufanyakazi ya ujenzi kwa mkurugenzi wa kampuni ya Lekuni ya wilayani Nzega matokeo yake badala ya kupata haki yake hiyo aliyokuwa akidai kama ujira kwa kazi aliyoifanya imedaiwa kuwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw.Silvesta Msele alimfyatulia risasi na kumjeruhi vibaya mguu huo.

Kamanda wa Polisi mkoani Tabora ACP Anthony Rutha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo mnamo tarehe 16 Desemba 2012 majira ya saa 12:45 jioni huko maeneo ya Kitongo wilayani Nzega.


Hata hivyo tukio hilo limeendelea kuzua malalamiko kwa baadhi ya wakazi wa wilayani Nzega huku wakitafsiri unyama wa aina hiyo umefanyika kutokana na kibri cha uwezo wa kifedha kwakuwa anayedaiwa kufanya unyama huo yupo mitaani akiendelea na shughuli zake huku majeruhi kijana Levis akiendelea kusota kwa kutibu majeraha aliyonayo ambayo yamesababisha kushindwa kuendelea na shughuli za utafutaji wa riziki yake ya kila siku.  


No comments:

Post a Comment