Sunday, January 27, 2013

VIJIJI VYAPAYAN MAJI SAFI NA SALAMA NZEGA DC

 
 NA LUCAS RAPHAEL NZEGA

MKUU  wa Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Bituni  Msangi amsema huduma ya maji vijijini  imeboreshwa kwa kiasi kikubwa hadi hadi  kufikia  asilimia 40% kutoka  asilimia 36% mwaka 2005. 

Akizungumza na waandishi wa Habari  jana Ofisini kwake alisema huduma hiyo ya maji safi na salama imepatikana kwa kuchimba visima virefu vya maji pamoja na visima vifupi ambavyo vimechimbwa katika kata mbalimbali za wilaya hiyo. 

Alisema kuwa hapo awari wananchi waishio vijijini walikuwa wakipata shida kubwa ya maji kutokana na uhaba wa vyanzo vya maji  nakuongeza kuwa vijiji vilivyo bahatika kupata visima hivyo vya maji vitumie kwa uangalifu miradi hiyo . 

Msangi alisema kuwa  Richa ya kuwa na 40% ya upatikanaji wa maji safi vijijini bado kuna uhaba wa maji kwa baadhi ya vijiji ambapo serikali imejipanga kukabiliana na tatizo hilo ilikuhakikisha wananchi wanapata maji kwa asilimia 100% hasa kwa kukamilika mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria hadi Tabora. 

Alibanisha kuwa katika miradi hiyo visima vilivyo chimbwa mwaka 2005 vilikuwa visima 472 ambapo mwaka 2012 visima hivyo vimefikia idadi ya 538 kati ya hivyo visima virefu ni 203 huku visima vifupi vikiwa 335. 

Amewataka wananchi wananchi wa wilaya ya Nzega kutuma visima hivyo kwa uangalifu ili kuepuka adha ya maji kwa musimu wa masika. 

Alisema serikali wialayani hapa imeweka sheria ndogo za kuhakikisha utunzaji wa vyanzo vya maji vinatunzwa pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata Elimu ya maji safi na salama ili kila mwananchi apate kuelewa ikiwa na kutunza vyanzo vya maji. 

Msangi alisema kuwa upatikanaji wa maji mjini ni kwa asilimia 59% kwa mwaka 2005 ambapo mwaka 2012 upatikanaji wa mjini ulikuwa 61% huku upatikanaji huo wa maji kwa ukiwa ni 40% kwa mwaka 2012 wakati mwaka 2005 ulikuwa 36%. 

Mwisho.


No comments:

Post a Comment